Thursday, March 4, 2010

HABARI ZA MAENDELEO YANGU KATIKA MASOMO YA UZAMIVU

Imehifadhiwa leo hii tarehe 5 Machi, 2010, nami Zainab M. Mwatawala.

1. Natanguliza Kumshukuru Mungu. Leo nina dhamira ya kuhitimisha taarifa ya malipo ya "Situational Analysis", niliyoyaomba tarehe 17/9/2009 kwa ajili ya kazi niliyoifanya kati ya tarehe 27/9/2009 na tarehe 10/10/2009 (yaani mwaka jana).

2. Hatimaye leo, baada ya "quarter" tatu za kutolewa mafungu ya fedha kupita, yaani ile ya Julai-Septemba, Oktoba-Disemba, na Januari-Machi. Leo ndio nimepokea fedha taslim kwa njia ya Hundi ya CRDB Bank (Mzumbe Branch) Na. 044685 ya tarehe 4 Machi, 2010, iliyolipwa kupitia Vocha Na. 103/3 ya tarehe 3/3/2010, ya Shilingi (Tshs.) 992,500/= (yaani kwa maneno ni: shilingi mia tisa tisini na mbili elfu, mia tano tu) kwa ajili ya kazi hiyo niliyoifanya kwa kutumia raslimali fedha binafsi wakati huo.

3. Pia habari nzuri nyingine ni kuwa HATIMAYE, Andiko langu la kitaaluma juu ya "Starting a Legal Aid Clinic at Mzumbe University", (Uanzishwaji wa Kituo cha Kutoa Msaada wa Sheria Chuo Kikuu Mzumbe - MULAC) ambalo nilisema hapo nyuma kuwa nililihadhirisha kwa hadhira ya Kitaaluma Chuo Kikuu Mzumbe tarehe 1/9/2009, nitalihadhirisha tena rasmi katika ngazi inayofuata ya Mkutano wa "Faculty of Law (FOL) Internal Examiners Board" utakaofanyika siku ya Jumanne, tarehe 9/3/2010 Chuo Kikuu Mzumbe.

4. Baada ya hatua hiyo muhimu katika ngazi ya mambo ya Kitaaluma Chuo Kikuu Mzumbe, Andiko hilo nitalihadhirisha katika Mkutano wa Bodi ya Kitivo cha Sheria (FOL Faculty Board utakaofanyika tarehe 11/3/2010, kabla ya bodi hiyo kuridhia ili lifikishwe katika kikao cha Seneti (senate) utakaofanyika tarehe 19/3/2010, Chuo Kikuu Mzumbe.

5. Mkutano wa Seneti ndio ngazi ya mwisho itakayopendekeza endapo Andiko hilo lipite au la; yaani kikao hicho kina mamlaka ya kulipeleka pendekezo la kuanzisha rasmi Kituo cha Kutoa Msaada wa Sheria Chuo Kikuu Mzumbe (MULAC) kwa Baraza la Chuo (Mzumbe University Council), litakalokutana tarehe 26/3/2010 Chuo Kikuu Mzumbe. Hii ni kwa mujibu wa Kalenda ya Kitaaluma (ALMANAC) Chuo Kikuu Mzumbe ya mwaka 2009/2010.

6. Namuomba Mungu anisaidie ili kusiwe na vipingamizi, vigingi, wala vikwazo vitakavyokwamisha kazi hii kusonga mbele kadri ya ratiba hiyo niliyoielezea.

No comments:

Post a Comment