Sunday, July 22, 2012

GREEN FOREST COBRA AGED 209 YEARS IN TANZANIA !!!!!

20 July 2012 - MAJIRA, TANZANIA. Serikali kumsaka nyoka mwenye miaka 209 Na Theonestina Juma, Bukoba SERIKALI imedhamiria kumsaka nyoka mwenye umri wa miaka 209 aliyepo katika Msitu wa Akiba Minziro, uliopo Wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera. Lengo la kumsaka nyoka huyo ni kutokana na ukongwe wake hivyo kuwa kivutio kikubwa duniani hasa katika sekta ya utalii. Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki nchini, Dkt. Felician Kilahama, aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari. Alisema nyoka huyo mwenye futi 47, atapatikana baada ya mapito yake katika msitu huo kuonekana ila ni vigumu kuonekana hadharani kwa sababu hupendelea kuishi mapangoni. “Huyu nyoka lazima tumfanyie mahesabu ya kumkamata kirahisi, umri wa miaka 209 sio mchezo, ameweza kutambulika Baada ya kupima urefu wa mapito yake, pia kuna chatu na nyoka wenye mapembe,” alisema Dkt. Kilahama. Aliongeza kuwa, licha ya nyoka kuhatarisha maisha ya watafiti lazima kufanyike uharaka wa kuupandisha hadhi msitu huo uwe hifadhi ya Taifa ili kuboresha usimamizi wake. “Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa Kagera (RCC), kilipitisha msitu huu upandishwe hadhi, nyoka huyu ambaye ni aina ya Giant Forest Cobra, kichwa chake kina rangi nyekundu na sehemu ya kiwiliwili rangi ya kijani. “Alianza kufanyiwa utafiti mwaka 2000 baada ya kupatikana kwa taarifa kutoka kwa wenyeji wa maeneo hayo juu ya kuwepo kwa aina ya nyoka huyo katika msitu huu,” alisema. Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Halmashauri ya Missenyi, kupitia Maofisa wa Misitu, mwaka 2010 walianza kuweka mitego ya sindano katika mapito anayotumia ili kuchukua damu yake na kwenda kuipima vina saba ndipo ilibainika kuwa hadi kufikia mwaka huo, alikuwa na miaka zaidi ya 207. Dkt. Kilahama alisema nyoka huyo atakuwa kivutio muhimu mkoani hapa kama atapatikana licha ya kukabiliwa na tatizo la ukumbwa wa msitu ambao hekta 25,000 kwani nyoka huyo amekuwa akihama mara kwa mara kwa ajili ya mawindo. Ofisa Misitu wilayani hapa, Bw. Wilbard Bayona, alisema nyoka huyo ana uwezo wa kuishi siku 68 bila kula chochote zaidi ya maji baada ya kumeza mnyama yeyote ambaye atamkamata mawindoni. -- http://majira-hall.blogspot.com/2012/07/serikali-kumsaka-nyoka-mwenye-miaka-209.html

FRUITS OF ZIMBABWEAN'S SELF DETERMINATION

In Zimbabwe Land Takeover, a Golden Lining - 21/7/2012 By LYDIA POLGREEN HARARE, Zimbabwe — When Roger Boka started his auction business in the 1990s, this city’s tobacco trading floors were hushed places, save the mellifluous patter of the auctioneer. A handful of white farmers, each selling hundreds of bales of tobacco, arrived in sport utility vehicles, checking into the city’s best hotels while waiting for their big checks to be cut. During this year’s auction season, a very different scene unfolded underneath the cavernous roof of the Bock Tobacco Auction Floors. Each day, hundreds of farmers arrived in minibuses and on the backs of pickup trucks, many with wives and children in tow. They camped in open fields nearby and swarmed to the cacophonous floor to sell their crop. The place was lively and crowded; two women gave birth on the auction floor. The most obvious difference, though, was the color of their faces: every single one of them was black. “You used to only see white faces here,” said Rudo Boka, Mr. Boka’s daughter, who now runs the family business. “Now it is for everybody. It is a beautiful sight.” Before Zimbabwe’s government began the violent and chaotic seizure of white-owned farms in 2000, fewer than 2,000 farmers were growing tobacco, the country’s most lucrative crop, and most were white. Today, 60,000 farmers grow tobacco here, the vast majority of them black and many of them working small plots that were allotted to them in the land upheavals. Most had no tobacco farming experience yet managed to produce a hefty crop, rebounding from a low of 105 million pounds in 2008 to more than 330 million pounds this year. The success of these small-scale farmers has led some experts to reassess the legacy of Zimbabwe’s forced land redistribution, even as they condemn its violence and destruction. The takeover of white commercial farms was a disaster for Zimbabwe on many levels. It undermined one of Africa’s sturdiest economies, and as growth contracted and its currency became worthless because of hyperinflation, joblessness and hunger grew. Large chunks of land were handed to cronies of President Robert Mugabe, many of whom did not farm them. It spurred a political crisis and violent reprisals by the security forces that have killed hundreds of people. Yields on food and cash crops plummeted. But amid that pain, tens of thousands of people got small farm plots under land reform, and in recent years many of these new farmers overcame early struggles to fare pretty well. With little choice but to work the land, the small-scale farmers have made a go of it, producing yields that do not match those of the white farmers whose land they were given, but are far from the disaster many anticipated, some analysts and scholars say. “We cannot make excuses for the way it was carried out,” said Ian Scoones, an expert on farming at the University of Sussex who has been intensively studying land reform in Zimbabwe for the past decade. “But there are many myths that have taken hold — that land reform has been an unmitigated disaster, that all the land has been taken over by cronies in the ruling party, that the whole thing has been a huge mess. It has not. Nor has it been a roaring success.” The result has been a broad, if painful, shift of wealth in agriculture from white commercial growers on huge farms to black farmers on much smaller plots of land. Last year, these farmers shared $400 million worth of tobacco, according to the African Institute for Agrarian Studies, earning on average $6,000 each, a vast sum to most Zimbabweans. “The money that was shared between 1,500 large-scale growers is now shared with 58,000 growers, most of them small scale,” said Andrew Matibiri, the director of Zimbabwe’s Tobacco Industry and Marketing Board. “That is a major change in the country.” The new farmers are receiving virtually no assistance from the government, which for years poured money into larger farms given to politically connected elites. Instead, farmers are getting help from the tobacco industry, in the form of loans, advances and training. It is in Ms. Boka’s interest to revive the industry, so the company has invested heavily in helping farmers improve the yields and quality. Tobacco is a tricky crop, requiring precise application of fertilizer and careful reaping. It must then be cured and graded properly to fetch a top price. Recently, Alex Vokoto, head of public relations at the auction house, spotted several bales of desirable tobacco leaves cured to a honey color on the floor, and hustled the man who grew them, Stuart Mhavei, into the V.I.P. lounge for a cup of coffee and a chat. “This man is growing top-quality tobacco, and he has only been at it for three years,” Mr. Vokoto said. Mr. Mhavei, a 40-year-old tile layer, got a small piece of a tobacco farm several years ago in the town of Centenary in central Mashonaland, about 80 miles from Harare. “All the big guys who got land, they are doing nothing,” Mr. Vokoto said. “But these small guys are working hard and really producing.” Mr. Mhavei has steadily increased his yield, quality and income. So far this season, he has earned more than $10,000 on part of a vast farm that once belonged to a white family, investing the profits in a truck to transport his tobacco, as well as renting the truck to other farmers. Mr. Mhavei said that like many of the other people who got land, he supports Mr. Mugabe and his party, ZANU-PF. “Why should one white man have all this?” he asked, sweeping an arm across the lush, rolling farmland around his fields. “This is Zimbabwe. Black people must come first.” Charles Taffs, president of the Commercial Farmers Union, said that the industry could have been transformed to include more black farmers in a much less destructive way. “The tragedy with tobacco is that expansion, if they had the right policies, could have been done in the 1990s in conjunction with the commercial sector,” Mr. Taffs said. Instead, hundreds of thousands of workers have lost their jobs and the country has suffered huge economic losses as a result. The personal cost for white commercial farmers has been immense. One white tobacco farmer in northern Zimbabwe whose family purchased its land after independence described the slow, painful erosion of his family’s livelihood. “Now that we are down to less than 200 hectares, there isn’t enough income to support everyone,” said the farmer, who asked not to be identified because he feared seizure of even more land if he spoke out. A plot of 200 hectares is less than 500 acres. His brother had to leave the farm to find work elsewhere, and his own future was deeply uncertain. The farm employs far fewer workers. Yields are down since critical investments in irrigation and other infrastructure have been put off, he said. “We are Zimbabweans,” the farmer said. “We employ people, and take care of our workers. It is really painful to see this happening to our country.” The tobacco yield is still below its peak in 2000, when the crop hit 522 million pounds. But Tendai Murisa, a researcher who has studied tobacco farming since land reform, said that judging the success of land reform by looking at production figures misses a crucial point. “No one ever argued that this is a more productive form of farming,” Mr. Murisa said. “But does it share wealth more equitably? Does it give people a sense of dignity and ownership? Those things have value, too.”

UAMSHO ZANZIBAR WAJIBU MAPIGO

IMEINGIZWA HUMU TAREHE 22/7/2012 Majibu ya Uamsho Zanzibar kuhusu kauli ya kwamba wamo serikalini. http://uamshozanzibar.files.wordpress.com/2012/06/zanzibar.jpg? Jana tulisikia kauli zenu na mukasema Uamsho wapo Serikali. Sisi tunayakubali maneno yenu na tunakiri kuwa ni kweli Uamsho wapo Serikalini. Ila nyinyi mumeshindwa kuwataja kwa majina sisi tutawataja kwa majina na vyeo vyao. Muamsho wa kwanza ni Rais Jakaya Kikwete. Yeye ametuamsha kwa kutwambia wazi Wazanzibari kuwa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba haitoratibu Muungano. Hivyo ametuamsha na kutuwekea bayana Wazanzibari kuwa Tume hiyo haituhusu, sisi Wazanzibar kinachotuhusu kwenye Katiba ni Muungano. Katuamsha kuwa Tume hii ya Katiba si ya Muungano. Kikwete huyo huyo ametwambia kuwa Muungano ushavunjwa na CCM NEC, na alisema NEC imeshaamuwa kuwa Rais wa Zanzibar asiwe Makamu wa Rais wa Muungano. Hivyo ametuamsha kuwa NEC imeenda kivyume na Hati ya Muungano na kwenda kivyume na makubaliano ni kuyavunja makubaliano, hivyo NEC imeuvunja Muungano. Muamsho mkubwa zaidi ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Yeye alituamsha pakubwa tena akatutowa kwenye usingizi mzito pale alipotwambia kuwa Zanzibar si Nchi. Hata alipoambiwa ni nchi amekosea, akasema: “Sijakosea wala sijalewa. Zanzibar si nchi.” Kwa hakika, Pinda ametuamsha pakubwa. Muamsho mwengine ni Mwalimu Julius Nyerere alipotwambia amechoka na sisi Wazanzibari; na hapa namnukuu: “Tumechoshwa na Wazanzibar i na Uislaam.” Kama si Muamsho, huyu ni nani? Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Marehemu Mzee wetu Abeid Amani Karume, alituachia uswiya kwamba “Muungano ni kama koti, likitubana tutalivuwa!” Naye pia ni Muamsho. Muamsho mwengine ni Mansour Yussuf Himid. Naye katuamsha si haba pale aliposema ndani ya Baraza la Wawakilishi kuwa serikali moja hataki kuisikia, mbili ni butu, anataka serikali tatu au vyenginevyo. Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita, Shujaa Amani Karume ndiye aliyezidi sio tu kutuamsha, bali pia akatuletea Umoja wa Kitaifa na Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya mwaka 2010 tena akaifanya iwe shoka la kuvunja Muungano. Isomeni vizuri Katiba ya Zanzibar na hapo mutajuwa kuwa Karume ni Muamsho au si Muamsho. Kwa hiyo, Stephen Wassira na UVCCM hamjakosea kusema Muamsho wapo Serikalini. Ni kweli. Tena wapo serikali ya Chama chenu. Wala msimtafute mchawi. Wachawi wenyewe. ---- http://uamshozanzibar.wordpress.com/2012/06/06/ni-kweli-uamsho-wamo-serikalini-jibu-la-vjana-wa-uamsho-kwa-wassira-na-uvccm/

Thursday, July 19, 2012

WAZIRI BERNARD MEMBE NA URAIS 2015

Urais 2015 wazidi kuwatesa wanasiasa Tuesday, 17 July 2012 21:33 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe MEMBE ASEMA HAJAOTESHWA KUGOMBEA, ATANGAZA ORODHA YA MAADUI 11, CUF YAONYA MAKUNDI CCM NI HATARI MBIO za kuwania urais wa mwaka 2015 zimezidi kuwatesa wanasiasa, baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kueleza kuwa hajaoteshwa kuwania kiti hicho, huku Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akionya kuwa makundi tofauti yanayowania nafasi hiyo ndani ya CCM ni hatari.Membe mbali na kusema hajaoteshwa kugombea urais, ameeleza kuwa ana orodha ya watu kumi na moja wanaomhujumu na kuonya kuwa ipo siku atawataja kwa majina hadharani. Waziri Membe alitoa kauli hiyo juzi usiku (15/7/2012) katika Kipindi cha Dakika 45, kinachorushwa na Televisheni ya ITV kila Jumatatu. Membe alihusisha hujuma hizo na mbio za Uchaguzi Mkuu wa 2015, baada ya kuulizwa ikiwa watu hao wanamfuatafuata kutokana na suala la Uchaguzi Mkuu ujao wa urais. “Wanajua mambo yote haya, wanaogopa nisiwaguse na wangekuwa na uwezo wangeanza kampeni, labda nioteshwe (urais) na ole wao nikioteshwa ndoto hiyo…” alisema. Waziri Membe na kuongeza: “Mtu aliye mbaya wako anakuwa na macho matatu. Kwa hiyo kutokana na uwezo wa jicho la tatu anaanza kuzuia lile analoliona lisitokee. Mimi nina macho sita. Nitawataja. Hebu wewe fikiria, kila baada ya miezi miwili naletewa mitego, vituko. Lakini nawaambia Watanzania, waache waseme na mimi ipo siku itakuwa zamu yangu nitawaweka wazi ili kila mtu aelewe.” “Wasije wakadhani wakijificha kwa wahariri, majumbani kwao ambako ndiyo kuna ofisi zao kwenye ma-godown (maghala) yao ndiyo watakwepa, nitawalipua ili wajue. Ukikaa juu ya nyoka, akigeuka atakuuma tu.” “Ipo siku nitawaanika hao watu na wapo kumi na moja. Kuna waandishi wa habari mle ndani wawili. Nitawatwanga peupe. Ninyi subirini hata ndani ya Bunge, nitazipangua tuhuma hizo moja baada ya nyingine. Nikimaliza bungeni wajiandae, nitawaanika majina yao, picha zao na mambo yote waliyoandika kwenye magazeti kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wangu kwenye wizara.” “Nilikwenda Brazil nikazungumza na Waziri wao wa Mambo ya Nje changamoto anazokumbana nazo akasema ni uongo. Nikamwuliza anapambana nazo vipi akanipa dawa ambayo ni kuwaanika. Nawaambia nitawaanika hapatakalika hapa.” “Unajua nchi hii kisiasa ina watu ambao wana nguvu nje ya mamlaka ambayo wanayatumia kuvuruga. Wanapenda tuwe na watu wanaovurugika, wasingependa kuona watu wametulia. Ikiwa utaamka na kusema leo nitajivua gamba, leo nitafanya hivi utaandamwa. Wapinzani na wabunge Akizungumzia siasa za vyama vingi, Membe alivikosoa vyama hivyo akivitaka viwe makini. “Naona bado hatujakaa sawa kwa siasa za vyama vingi. Ni kweli, tuna vyama vya upinzani lakini inabidi viwe makini. Kitu ambacho wapinzani hawajui ni kwamba nguvu ya wananchi inaweza kubadilika saa 24, nguvu ya wananchi iko kama bahari ina mawimbi ya kupanda na kushuka,” alisema. Alisema vipo baadhi ya vyama vya upinzani barani Afrika, vilivyoingia madarakani na kuanguka akisema vilishindwa kutambua nguvu ya wananchi. Aliwataka wabunge wa upinzani kutumia muda wao mwingi kuangalia majimbo yao badala ya kusema tu bungeni. “Wapinzani ‘reference’ yao iko majimboni siyo bungeni. kipimo chako cha kazi ni jimboni, siyo ukasuku wa kuzungumza bungeni na waandishi wa habari. Nendeni jimboni kwake mkaone uchungu alionao. Lakini siyo anatumia asilimia 100 kuisemea dunia na nchi nzima huku amelisahau jimbo lake,” alisema. Aliwakosoa pia wapinzani kwa kukosoa bajeti halafu baadaye wanawafuata mawaziri kuwaomba fedha zilizotengwa. “Nakwambia naomba tupitishe hizo pesa, unakataa, halafu kesho unakuja na kusema katika hizo pesa ulizopitishiwa naomba kwa ajili ya miradi ya maji,…” Uendeshaji Bunge Kuhusu uendeshaji wa Bunge, Membe alisema hakuna tatizo ingawa aligusia kuwepo kwa ushabiki ulioibuka ambao alisema unalipeleka pabaya. “Viongozi wa Bunge wanafanya kazi nzuri ila huu ushabiki unaofanywa na ubabe usipodhibitiwa tutaliharibu. Nawaambia Watanzania ukiona mbunge anatumia muda mwingi bungeni kuliko jimboni, jibu ni moja tu, kumwondoa.” CUF nayo yanena Wakati Membe akisema hayo, Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), limetoa tamko na kuonya kwamba mpasuko wa kisiasa ndani ya Serikali ya CCM, unaathiri na kuyumbisha nchi kikisema umesababisha makundi ambayo yanapambana kuwania nafasi ya kugombea urais ifikapo 2015. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema hayo Dar es Salaam jana alipokuwa akieleza maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wa Taifa la chama hicho ambayo yaliitaka Serikali ya CCM kuacha kuyumbisha nchi kwa kuangalia suala la urais 2015. Profesa Lipumba alisema jukumu la msingi la chama kinachounda Serikali ni kufahamu kwamba nchi inahitaji mabadiliko ambayo yatawaletea maendeleo wananchi na huu si wakati wa kujadili nani anatakiwa kuwa Rais mwaka 2015, kwani hiyo ni njia ambayo inaweza kuwagawa Watanzania. Bajeti bado tatizo Kuhusu Bajeti ya Serikali, Profesa Lipumba alisema kikao cha Baraza Kuu kimebaini kuwa malengo ya Bajeti ya 2011/2012 hayakufikiwa kwani mfumuko wa bei umezidi kuongezeka tofauti na Serikali inavyoeleza kwamba umepungua. “Takwimu zinaonyesha kwamba wakati Waziri wa Fedha anasoma hotuba ya Bajeti Juni, 2011 mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 10.9 na uliongezeka hadi kufikia asilimia 20 na kwamba mwishoni mwa mwaka 2011, ulipungua kidogo hadi kufikia asilimia 18.2 lakini bado ni tatizo kwa wananchi kwani wanaendelea kuteseka na hali ngumu ya maisha kutokana na bei za bidhaa kuendelea kuwa juu,” alisema. Alisema katika kukabiliana na upungufu wa umeme, Serikali iliahidi kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 100 Dar es Salaam pamoja na megawati 60 Mwanza lakini mpaka sasa hakuna dalili yoyote ya kukamilika kwa miradi hiyo. “Serikali ilisaini mkataba wa kupewa mkopo wa Euro 61 milioni na benki ya HSBC. Mkopo huo ulielekezwa kugharimia ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa megawati 60 Nyakato, Mwanza lakini cha kushangaza bajeti tano mfululizo zimekuwa zikitoa ahadi kama hizi bila utekelezaji,” alisema na kuongeza: “Serikali ya CCM imeshindwa kutatua matatizo ya umeme na kuisababishia nchi kupata hasara na kudhoofisha uchumi.” Akizungumzia ushiriki wa chama hicho katika uchaguzi wa marudio ya Ubunge katika Jimbo la Bububu, Zanzibar alisema CUF kimeridhia kushiriki kwani hiyo ni ngome yake kubwa na kimejipanga kushinda. Imeandikwa na Elias Msuya, Aidan Mhando na Vicky Kimaro

AINA MPYA YA WIZI DAR ES SALAAM, TANZANIA

From: Shufaa Alwiy To: shaibumatessa@yahoo.com Sent: Tuesday, July 10, 2012 11:37 PM Subject: Fw: Wizi mpya Dar-es-salaam STYLE YA KWANZA Hi Everyone, I hope you are well. I am writing this email because of an incident that happened to my dear friend on 6th July 2012 at Mlimani City, Dar-es-salaam.TZ. Mtu asiemjua alimsimamisha kwa kumuita kwa jina lake Mlimani city wakati amemaliza shopping (muda wa saa mbili kasoro usiku baada ya kutoka kazini). Yule kaka akajaribu kumkumbusha matukio mbalimbali ya huko nyuma (kama mtu anayemfahamu). Anasema alisogea restaurant kununua maji na hilo ndio tukio la mwisho analolikumbuka. Saa saba usiku amerudishwa nyumbani kwake na gari yake akiwa bado hana fahamu. Wamemchukulia simu, hela na baadhi ya hela zimetolewa kwenye ATM machines. Thank God hawakudhuru kabisa. Ila kinachoogopesha ni kwamba huyu mtu alikuwa anajua historia yake (ndugu zake na marafiki zake) na anajua anapoishi. It is very disturbing. Naomba mufahamishe ndugu na marafiki zenu kuhusu tukio hili. Ubinaadamu haupo tena kwahivyo tuwe makini tukiwa tunatembea huko mitaani...I hope this email will help others to avoid such tragedies!! Please forward this email to your friends and families! Shufaa STYLE YA PILI From Andrew Peter Kato Kuna utapeli wa aina nyingi sana hasa parking ya Mlimani City! Wenye magari kuweni makini sana! Juzi naingia kwa gari naondoka jamaa akanifuata ati anataka msaada nikamwona mapema kabisa anavyobadilisha sura ili aoenekana mhitaji msaada! Nikamuwahi nikafunga vioo! Nikashusha kidogo nikamhoji akadai ati anaomba japo nauli arudi gerezani! (Just imagine the way he confused himself kwani nilimchenjia ni balaa) Sasa gerezani umetorokaje, kwanza huna uniform, then umefanikiwa kutoroka bado unataka urudi, LOL! Nilipotafakari na kumsimulia jamaa yangu akadai ndiyo janja yao, anakuomba msaada na ukishampatia anakushukuru kwa kukupa mkono, hapo ndipo inakuwa imekula kwako kwani wana kitu cha nja kali kama kisindano kidogo wanakuchoma nacho mnapopeana mkono then from there unapoteza fahamu, na ndipo wenzake wanatokea. Unapakiwa kwa gari wakidai ndugu yao kazidiwa, unapelekwa kusikojulikana, wazee wanasepa na gari! BEWARE tupunguze ukarimu waTZ, wema usizidi uwezo!

HII NI LAANA YA UKOSEFU WA MAADILI YA UDAKTARI

Saturday, March 12, 2011 HII NI LAANA YA UKOSEFU WA MAADILI Imeandikwa na Neema Kidumba, MIJO, Mbeya; Tarehe: 10th March 2011 Habari Leo TANZANIA. MTU anayetarajiwa kuepusha madhila kwa mwingine kutokana na taaluma yake kumbe anaweza akafanya kinyume chake na kuwa chanzo cha madhila hayo. Taswira hiyo ndiyo imejitokeza mkoani Mbeya ambapo daktari ambaye alitarajiwa kuwa mwadilifu na kuhakikisha hasababishi matatizo kwa si tu mgonjwa lakini hata mtu mzima, ameshindwa kufanya hivyo. Daktari Mfawidhi wa Hospitali ya Wazazi Meta mkoani hapa, Moses Achiula (57) ndiye aliyefanya hayo na hatimaye kujikuta akianza kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukiuka maadili yake. Dk Achiula amepatikana na hatia ya kumnajisi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11 na kumwambukiza virusi vya Ukimwi(VVU). Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa, Michael Mteite ambaye alisema Mahakama pia imemwamuru daktari huyo kulipa faini ya Sh. milioni mbili. Awali ilidaiwa mahakamani hapo na waendesha mashitaka, mawakili wa Serikali Giriffini Mwakapeje na Francis Rojas, kuwa mshitakiwa alibainika kufanya kitendo hicho Januari 21 mwaka jana. Kwa mujibu wa madai ya waendesha mashitaka hao, Dk. Achiula alikuwa akimfanyia msichana huyo kitendo hicho mara kwa mara na siku aliyothibitika, ilikuwa ni mara ya tatu. Ilielezwa kuwa mshitakiwa alikuwa akimwita msichana huyo anayesoma darasa la nne nyumbani kwake eneo la Forest jijini hapa na kumwomba amfanyie usafi katika nyumba aliyokuwa akiishi peke yake. Lakini inadaiwa kuwa baada ya mtoto huyo kumaliza shughuli aliyoombwa kuifanya, daktari huyo alikuwa akimlazimisha kufanya naye ngono. Waendesha mashitaka hao walidai kuwa daktari huyo pia alikuwa akimwambia mtoto huyo akiona wazazi wake wakiondoka, aende nyumbani hapo na kumtisha kuwa asipokwenda, atamwua. Wakati akitenda unyama huo kwa msichana huyo mdogo ambaye kiumri ni sawa na mjukuu wake, inadaiwa daktari huyo alikuwa akimtishia kumpiga iwapo angelia au kupiga yowe kuomba msaada. Waendesha mashitaka walidai kuwa baada ya kumaliza kumfanyia unyama huo, daktari huyo alikuwa akimpa fedha kidogo, ili asieleze kilichokuwa kikiendelea kwa mtu yeyote. Ilidaiwa kuwa siku ya kwanza, daktari huyo alimpa Sh. 1,000, siku ya pili Sh. 500 na siku ya tatu Sh. 200 na ndipo msichana huyo alipoamua kutoa siri kwa wazazi wake waliochukua hatua za kisheria. Walisema baada ya wazazi kulifikishwa suala hilo panapostahili, msichana huyo alipelekwa katika Hospitali Teule ya Ifisi kwa ajili ya uchunguzi na kukutwa ameambukizwa magonjwa ya zinaa vikiwamo virusi vya Ukimwi. Hakimu Mteite alisema ametoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama ya daktari huyo. Posted by Zainab Mrisho Mwatawala at 11:41 PM No comments:

Tuesday, November 8, 2011

ATI? WATANZANIA WANATAMANI KUWA WAMAREKANI !!! WATUULIZE TULIOFIKA NA KUISHI HUKO !!!

Watanzania wanatamani kuwa Wamarekani
Saturday, 05 November 2011 21:31


Na Assumpta Nalitolela, Gazeti la Mwananchi, Tanzania.

KUIGA kutoka kwa mtu aliyefanikiwa ni jambo jema, tena linakubalika pale ambapo mbinu safi zilizomfanya mhusika afanikiwe, ndizo zinazoigwa. Hivyo hata katika biashara, mtu anatakiwa ailinganishe biashara yake na ile yenye mafanikio na aangalie ni kipi anaweza kuiga na kukiingiza kwake ili naye apate mafanikio.

Vijana wanaaswa waige kutoka kwa watu wazima ambao wamekuwa na mafanikio ili nao wafuate nyayo. Hivyo kuiga kupo na ni jambo jema. Kwa kulikazia hilo kuna msemo kwamba ‘‘kwanini uhangaike kuunda gurudumu wakati tayari kuna mtu aliyekwisha liunda?’’ Huko ni kupoteza raslimali muda ambayo inahitajika sana kwa mambo mengine ambayo katika dunia hii yapo mengi.

Hivyo kuiga kwa ajili ya maendeleo mimi hakunisumbui, kinachosumbua moyo wangu ni kuiga kulikopitiliza kiasi kwamba mtu anatamani sio tu kuiga bali awe nakala ya huyo mtu anayemuiga. Kama ni suala la mtu moja moja tunaweza kusema mtu anaiga kwa kiasi ambacho anatamani kuwa nakala ya mtu mwingine, hiyo ni kumkosoa Mungu kwa kukuumba kama ulivyo.

Sijui tusemeje kama ni taifa ndilo linalotamani kuwa taifa jingine katika nchi yake yenyewe. Hapa ndipo tulipofikia Watanzania. Tunapenda kuwa Wamarekani tukiwa ndani ya Tanzania. Hali hii ipo toka kwa wasomi mpaka wasioingia darasani, taasisi binafsi mpaka zile za umma, wasanii mpaka wale wa fani zingine. Tulitafakari hili.

Sarafu ni alama moja wapo inayotambulisha taifa. Matumizi ya sarafu katika biashara kwa wakazi wa mahali fulani yanamuongoza mtu kusema kwa uhakikia kwamba, yupo kati ya watu wa taifa fulani.

Hivyo kama ni Shilingi ya Kenya, anajua kwamba yuko ndani ya mipaka ya Kenya. Kama ataigundua kuwa ni Shilingi ya Tanzania basi atajua yuko ndani ya mipaka ya Tanzania.

Umezuka mtindo ambao unakera kweli kweli; na nashukuru umma wa Watanzania umeanza kuupigia kelele, nao ni baadhi ya watu au taasisi kudai malipo kwa Dola ya Marekani badala ya shilingi kwa bidhaa na huduma wanazotoa. Hivi bila aibu mtu au taasisi inamdai Mtanzania kulipia bidhaa au huduma kwa dola katika nchi ya Tanzania, azitoe wapi na yuko kwenye uchumi wa shilingi?

Cha ajabu, haya yanafanywa hata na vitengo vya vyuo na shule ambako ulitegemea kuna wasomi wenye kuelewa vizuri kwamba sarafu ya nchi hii ni shilingi na kwamba ni shilingi ndio inayotakiwa kulindwa kwa sababu ndio yetu.

Shilingi ndio inayotutambulisha utaifa wetu. Sasa hata wasomi wanapokataa kuipokea maana yake nini? Kwamba tuingie kwenye mchakato wa kubadilisha sarafu ili tutumie Dola ya Marekani na Benki Kuu yetu iwe hiyo ya Marekani? Wasomi hawa wanatambua kwamba kudai kwao malipo kwa dola kunazidi kuizorotesha shilingi, cha ajabu hili haliwasumbui.

Natambua uimara wa dola na utamu wake katika biashara kwa mtu anayeipokea lakini hiyo sio yetu. Tutafute mbinu za kuimarisha ya kwetu. Kuibeza pesa yetu kwa kuwa ni hafifu, ni sawa na mtoto kumbeza baba yake kwa kuwa hali yake hailingani na baba wa nyumba jirani.

Jambo lingine linaloonesha matamanio yetu ya kuwa Wamarekani ni mahangaiko ya vijana wetu ya kuwa na lafudhi ya Kimarekani na kuikataa ya makabila ya Kitanzania. Lafudhi hujengeka katika matamshi ya mtu kwa muda mrefu sana. Mtu hujengeka kwa lafudhi ya jamii inayomzunguka kipindi anachokua. Hivyo akikuzwa katika mazingira ambayo watu wanazungumza kwa lafudhi ya Kihaya ya kwake pia itakuwa ya Kihaya, vivyo hivyo Kinyakyusa, Kingoni nk. Baada ya kujengeka sio rahisi kutoka.

Lafudhi sio kitu kibaya, hiki ni kitambulisho cha jamii aliyotoka mtu. Kuikataa lafudhi ni kuikana jamii iliyomkuza. Vijana wanahangaika kutumia lafudhi ya Kimarekani wakati wanapoongea Kiingereza kiasi kwamba wanaishia kumung’unya maneno, yasiyoeleweka.

Hawaeleweki kwa sababu wanajaribu kuzungumza kwa namna ambayo sio wao. Lafudhi ya mtu ipo palepale haijalishi kama mtu huyo anaongea Kiswahili, Kingereza, Kichaga nk. Hivyo mtu anapojaribu kuibadilisha kwa kuwa tu anaongea lugha ya mtu mwingine, lazima itampa shida, na ataishia kuchekesha watu.

Uigizwaji wa lafudhi tunawaachia wasanii katika michezo ya kuigiza kwani lengo lao ni kutuchekesha. Kwa lafudhi yako mtu unajulikana unatokea upande upi wa dunia, kwa lafudhi yako unapendeza, kwa lafudhi yako mtu unajiamini zaidi unapoongea, lakini kwa lafudhi ya mtu mwingine unachekesha na hueleweki. Yanini mtu uishie kuwa kichekesho wakati hiyo haikuwa nia yako?

Tunatamani kuwa Wamarekani mpaka tunapeperusha bendera yao katika nchi yetu. Kama ilivyo kwa sarafu, bendera pia ni alama ya taifa. Tanzania tunapeperusha bendera ya Marekani kwa kubandika kwenye mikokoteni, kuvaa kama vilemba, kuibandika kwenye daladala, kuitangaza kwenye fulana tunazovaa.

Hiyo ni kutamani kuwa Wamarekani , hiyo ni kasoro kubwa sana kwenye taifa letu ambalo tunasherehekea miaka 50 ya kuwa huru. Miaka 50 ya kuwa na bendera yetu wenyewe ambayo sasa tunaikana na kutamani kupeperusha ile ya Marekani.

Haya ni machache tu yanayoashiria kulikana taifa letu la Tanzania. Ukweli nchi yetu ni maskini na ni ukweli tuna kasoro nyingi za hapa na pale zinazorudisha maendeleo ya nchi nyuma, lakini kusahihisha kwake sio kwa kuikana kwa kuendelea kuzorotesha uchumi kwa kutumia sarafu isiyo yetu, au kwa kutumia lafudhi isiyo yetu au kwa kuukana uhuru wetu kwa kupeperusha bendera isiyo yetu.

Tuchangie kwa kuhakikisha nasi tunakuwa taifa ambalo wengi wa watu wake wanaishi maisha yenye neema. Tukosoane, tuwajibike na tuige mambo ambayo mataifa mengine wameyatekeleza na kuwafanya waneemeke. Lakini tubaki kama Watanzania. Kwa wale wanaoukana Utanzania wao basi wahame wakaishi na jamii za taifa hilo wanalolipenda .

Tukutane Jumapili ijayo panapo majaliwa.


CHANZO: MWANANCHI