Saturday, October 3, 2015

WAFANYAKAZI WA SEKTA ZA AFYA WATAKA MABADILIKO TANZANIA !!!

* Kutoka Kagera, Katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wauguzi (Annual General Meeting).
Leo tarehe 30 Sept. 2015


* MADAKTARI, WAUGUZI, WAFAMASIA NCHINI WAUNGA MKONO RASMI VUGUVUGU LA MABADILIKO NCHINI.

Taarifa Maalumu Kwa wadau wa afya nchini (Wataalamu wa afya na wananchi wote). MUHTASARI:

Ndugu wananchi, na wadau wa afya nchini sisi viongozi wa Jumuiya ya Madaktari, nchini (MAT), Jumuiya ya Wauguzi nchini (TANNA) Jumuiya ya Wafamasia nchini (PST), na Association of Medical Practitioner of Tanzania(AMEPTA) nchini, tumekutana na kujadiliana mambo kadha yanayohusu mstakabali wa maendeleo mahususi ya sekta ya afya Kama wadau wa maendeleo,
AJENDA YETU: Afya kuelekea uchaguzi mkuu.

Tumechukua hatua hii madhubuti Kwa nia njema kabisa tukitambua kuwa sekta ya afya inakabiliwa na changamoto nyingi na zinahitaji hatua ya dhati kuinusuru sekta ya afya kuendelea kutoa huduma isiyokidhi viwango, kwani tunapojadili mstakabali wa afya za watanzania, tunajadili mstakabali wa harakati za taifa letu kujikwamua kutoka hatua hii ya maendeleo tuliofikia kwenda hatua nyingine iliyo bora zaidi, Kwa kadiri ya dira ya maendeleo nchini na duniani kwa ujumla.

* Kwa nini tunachukua hatua hii wakati tuko katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu ifikapo tarehe 25/10/2015,

Jibu: Ni kwamba tunatambua mustakabali na msingi wa mabadiliko ya kweli katika sekta ya afya na hata sekta nyingine za umma umo mikononi mwa Wanasiasa tunaoenda kuwachagua kuanzia madiwani, wabunge na raisi. Hivyo tungependa(Wahudumu/Wataalamu wa afya na wananchi wote watambue wanapoamua kuacha kupiga kura, au wanapopiga kura basi wanaamua mstakabali wa afya yao katika kipindi cha miaka mitano(5) ijayo au zaidi.
wote nchini tusifanye makosa, tuamue afya yetu sasa, tuchague kwa makini, tuchague mabadiliko ya kweli.

Aidha, TUNARIDHISHWA NA TUNAUNGA MKONO VUGUVUGU LA MABADILIKO NCHINI Kuelekea uchaguzi mkuu ifikapo tarehe 25/10/2015. "Afya bora Kwa wote inawezekana Tanzania" Tuamue tarehe 25 Octoba. "Tuchague mabadiliko"

Zipo changamoto zinazoikabili sekta ya afya 

1. Uhaba wa dawa na vifaa Tiba:
Hii inatokana na bajeti finyu ya sekta ya afya, hatuna viwanda vikubwa vya kuzalisha dawa nchini vinavyomilikiwa na serikali, Tanzania kuna msambazaji mmoja tu wa dawa nchini, yaani bohari kuu Kwa vituo vyote nchini huku akiwa hana uwezo wa kutosha kumudu kazi hii muhimu sana. Hii hufanya Wagonjwa au wateja wa huduma kulazimika kuandikiwa dawa ili wakajinunulie kwingineko.

Aidha, watalamu wa afya wanalaani na kuwasihi wanasiasa kuacha mara moja kueneza propaganda kuwa wahudumu wa afya wanaiba dawa, hivyo kusababisha upungufu wa dawa nchini, wakati inajulikana wazi upungufu wa dawa unatokana na ufinyu wa bajeti ya serikali katika sekta ya afya na si vinginevyo, aidha, kauli hiyo imewasikitasha na kuwapunguzia heshima na morali wa kazi wahudumu wa afya nchini.

2. Uhaba wa wafanyakazi wataalamu wa afya Kwa asilimia 56%, yaani chini ya nusu ya hitaji: 
 Mfano Kwa mwaka 2014, daktari mmoja alihudumia wagonjwa 20,000(1:20,000) badala ya daktari mmoja kubudumia wagonjwa 5000(1:5000). Matokeo yake mzigo wa kazi unakuwa mkubwa na unadhifu wa kazi unapungua.

3: Mazingira magumu ya kufanya kazi, Miundombinu mibovu,
hadi Leo mwaka 2015 wapo watanzania wanaolala chini hospitalini, na wengine wanaruhusiwa ikiwa hawajapona vizuri ili kupisha nafasi Kwa wagonjwa wengine.
Je, watanzania ni kwanini tusitamani mabadiliko?

Mpango wetu;
Nafasi ya wananchi kuelekea uchaguzi mkuu
Sisi tunatumia fursa hii adhimu kuwakumbusha watanzania wote, kama wadau wa afya na wadau wa maendeleo wajue wanapopiga kura, au wanapoacha kupiga kura basi, wanaamua afya zao, wanaamua hatima ya elimu yao, wanaamua uchumi wao na ustawi wa taifa letu Kwa pamoja. Ni muhimu kila mtanzania aliyejiandikisha ahakikishe anapiga kura, achague mabadiliko ili kusaidia kupata viongozi bora watakaosaidia kutatua kero zetu Kwa pamoja Kama taifa.

Matatizo mengi ndani ya sekta ya afya na hata sekta nyingine zinaweza kupunguzwa au Kwisha kabisa, tukumbuke baada ya uchaguzi huduma Kama afya, Elimu na nyingine nyingi hazitolewi Kwa itikadi ya vyama, tusichague kiongozi kwa mazoea ya chama(chetu), tuangalie je wanaweza kutusaidia Kama taifa?

Tukifanya makosa viongozi wasiofaa wakashinda, basi kulala chini hospitalini kutatuathiri wote, na kutaendelea daima, ilimradi tuko masikini. Ndugu zetu wanafunzi wakitanzania kukaa chini darasani kutawahusu pia, (tuamue sasa).

Tunahitaji viongozi wenye kuthubutu, Wenye dira, Maamuzi magumu, na Nguvu ya kusukuma mbele maendeleo yetu Kama taifa.

Dr. P. Magesa

No comments:

Post a Comment