Wednesday, March 12, 2014

UTHIBITISHO WA MAKATAZO YA MWENYEZIMUNGU JUU YA USHOGA WA KAUMU LUT


Posted here Today 12/3/2014.
 
TMA  [TANZANIA]  WAUKATAA   USHOGA
 
Rais wa Tanzania Medical  Association [TMA], Dr Primus F Saidia, ametoa statement ndeefu (published in Jamhuri - Mdosi, naomba tupeperushie), kupinga ushoga, baadhi ya hoja muhimu ni hizi hapa:
MOSI: Kuzaliana - kama jinsia zitaoaana zenyewe kwa zenyewe watoto hawatozaliwa, mwisho wake binadamu tutamalizika.
PILI: Ushoga haulingani na mfumo wa maisha ya kawaida ya Mwafrika, tukiiga hivihivi mfumo wa Kimagharibi, kuna matokeo ya kisaikolojia na kisoshiolojia ambaye hayatabiriki.
TATU: ushoga unaleta ukimwi. Ukimwi ulizaliwa Magharibi kutokea kwa mashoga.
NNE: katika mapenzi ya kawaida wanawake wanapotaka mapenzi, mwili hujitayarisha kwa kuweka lubrication before and after the event. Kwa mashoga, wanaume wanaoingiliwa huwa hawana kinga hiyo kwa sababu hawana lubrication. Hii inatoa mwanaya wa maambukizi yasiyotabirika.
TANO: magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende nchi za Magharibi yalishaisha, sisi yapo. Kisonono au kaswende kupitia njia za haja kubwa kwa mwanaume madhara yake yatakuwa makubwa na hayatabiriki.
SITA: magonjwa ya ini. Kuna ugonjwa unaitwa hepatitis A, B  na C. Virusi B na C huenezwa kwa njia ya damu, na virusi vya A huenezwa kwa njia ya mdomo na haja kubwa. Hepatitis A palepale inawaingia mashoga. Uchunguzi USA 1992 unaonyesha kuwa mashoga wana maambukizo 22% ya ini kuliko kawaida, ikiwemo kusinyaa kwa ini, kansa ya ini, na ini kushindwa kazi hadi kifo.
SABA: maradhi ya tumbo. Mashoga wanaathirika na ugonjwa uitwao GAY BOWEL SYNDROME kwa sababu ya khamisha bakteria kutoka sehemu moja ya utumbo kwenda sehemu nyingine ya utumbo wasikohitajika, huleteleza typhoid, herpetic ulcers, kanza ya maeneo ya mdomo na za eneo la haja kubwa.
NANE: je ushoga ni tabia ya kurithi au ya kuiga? Tofauti ya mwanaume na mwanamke ni hormones za kijinsia. Kila mtu ana homoni za kike na za kiume kwa kiasi mbalimbali, kwa wanawake homoni za kike ni nyingi zaidi na kwa wanaume hivyo hovyo lakini kwa asilimia tofauti tofauti. Kwa hiyo uwepo tu wa homoni za kike kwa mwanaume au za kiume kwa mwanamke si ajabu, na si sababu ya kusema uishoga unarithiwa. "UKWELI NI KUWA USHOGA NI TABIA ZA KUJIFUNZA KAMA TABIA ZINGINE ZOZOTE". Inaweza kuepukika kwa muhusika kuamua kuachana na msukumo. Ikumbukwe kwamba hata wanaume na wanawake wasio mashoga hupata hamu ya kujamiaana , lakini kwa kujizuia utawakuta wanajamiaana kwa utaratibu, kwa faragha, na si kusukumwa tu na hamu ya kutaka kujamiiana. Ni bahati mbaya watoto hujifunza mambo kama haya wakati wa kubalehe na kuvunja ungo. Iwapo mtoto ataanza kujifunza tabia ya ushoga ni vigumu kumrudisha kwa njia zingine, sawa tu na yule asiyefanya ushoga kumpeleka kwenye ushoga baadaye. TUNAWEZA KUEPUKANA NA TABIA ZA USHOGA KAMA TUKIWZA KUZUIA WATOTO WETU KUJIFUNZA USHOGA HASA KATIKA VIKUNDI NA SHULE ZA BWENI.
"Kwa kuhitimisha, nasema kwamba kwa upande afya ya kijamii, nchi zetu changa zina matatizo mengi ya kushughulika nayo. Mfani ni vifo vy watoto na kina mama, TB na mapafu, malaria, ukimwi na mengineyo mengi, bila kusahau magonjwa yasiyokuwa ya kuambukizwa kama kisyukari, presha, kiharusi na mengine lukuki. Wenzetu wa Magharibi walishayatokomeza ay kuyapunguza sana, ndiyo maana wanapata muda wa kujadili na kuyaendekeza masuala ya ushoga na pengine kuwakinga mashoga wao na maradhi. Sisi bado, tuliyonayo yanatutosha, hili la mashoga tuwaachie wao.
 
HONGERA   NYINGI   SANA KWA UTHIBITISHO HUU KUTOKA KWA WATAALAMU  WA TIBA NCHINI TANZANIA KUHUSU SUALA HILI LA  KUMKUFURU  MWENYEZI MUNGU.  [Mwenye Blogu]

No comments:

Post a Comment