Imetundikwa hapa leo hii 18/10/2013.
MSHAHARA WA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA WAZIRI MKUU WAKE - KUTOKA "MWANANCHI"
Jamani
sijui kama mmeisoma hii nimeiona kwenye Mwananchi ya tarehe 14 Oktoba, 2013; ambapo Mheshimiwa Mbunge Zitto Zuberi Kabwe
ameufichua mshahara wa Rais wa Tanzania kuwa ni shilingi milioni 32 kwa
mwezi au dola 240,000 kwa mwaka, wakati Waziri Mkuu wa Tanzania, analipwa shilingi
milioni 26 kwa mwezi. Zitto amesema hizi hazikatwi kodi hata senti tano,
na hawa viongozi wanapewa mahitaji yao yote na serikali.
This is sickening. It is blasphemous kwa Rais wa Tanzania ambaye
wananchi wake hawana dawa ya malaria, watoto wana kwashakor, shule
hazina madawati, ambaye anapita na bakuli kuomba 43 percent ya bajeti ya
serikali toka kwa Wazungu, huku take-home yake inazidi ya Rais wa
Marekani (USA) ambaye ni Barack Hussein Obama kwa sasa; ambaye analipwa 400,000$ kwa mwaka na zinakatwa kodi na mengine
mengi tu.
Have we no shame, no shame at all? If this is not institutionalized
thuggery I dont know what is? The President gets more than 1 million
shillings a day for 10 years straight while 40 percent of his people
live on less than $2 a day? Tuna uroho kiasi gani? Ni za nini wakati
kiinua mgongo chake ni 90 percent ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani
kwa maisha yake yote?
Our leadership has trully become immoral. I cringe to refer to these as
"leaders". 32 million a month kwa mtu anayetunzwa na kulishwa yeye na
familia yake kwa maisha yake yote?
Labda ndio maana wanafanya hii mishahara ni siri.