Wednesday, July 24, 2013

OMAR ADAM SYKES AAGWA NA MEYA WA WASHINGTON DC, U.S.A. VICENT CONDOL GRAY



Wednesday, July 10, 2013

MEYA WA DC KUONGOZA MAELFU KUMUAGA MAREHEMU  OMAR ADAM  SYKES; CHUO CHAFUNGUA OMAR SCHOLARSHIP FUND

Na Swahili TV, Washington DC

Chuo Kikuu cha Howard  alichokuwa akisoma mtanzania aliyeuawa  mjini Washington Dc,  marehemu Omary Adam Sykes kinataraji kuuaga mwili wake  leo jioni, viongozi mbalimbali akiwemo meya wa jiji la Washington DC Bwana Gray nao wanatarajiwa kuhudhuria.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia Swahili TV shughuli za kumuaga  marehemu zitafanyika katika ukumbi wa Andrew Rankin Memorial Chapel ulio katika kona ya  6th Street  na Howard place na kufuatiwa  sherehe za kukumbuka ya  maisha yake zitakazofanyika katika ukumbi wa Blackburn ambao pia uko katika chuo hicho.

Shughuli za kuuaga mwili huo zimepangwa kuanza saa 12 jioni (6pm), ambazo habari hizo zinasema Mstahiki meya  Vicent condol Gray atakuwa muongeaji mkuu akishirikia na rais wa chuo hicho  Profesa Sidney A. Ribeau. Sherehe hizi pia zitashirikisha familia ya marehemu Omar ambaye baba yake mzazi mze Adam Sykes  na baba yake mkubwa waliingia jana wakitokea nchini Tanzania.

Si jambo la kawaida kwa Meya wa jiji kubwa la Washington  kuhudhuria sherehe za kuuga mwili, wachambuzi wa mambo ya siasa za Washington Dc  wanasema  hali  hiyo huenda inatokana na umaarufu wa chuo hicho na mstuko mkubwa wa mauaji ya mwanafunzi  huyo ambayo yamelistua jiji la Washington DC,  ambalo licha ya kuwa na matukio ya mauaji ya hapa na pale  lakini eneo la chuo hicho limekuwa salama kwa miaka mingi.

Taarifa ya chuo kwa Swahili TV inasema,Uongozi wa chuo uliamuwa kuanzisha mfuko maalum utakaosaidia wananchi mbalimbali wasio na uwezo kulipia ada zao, mfuko utatambulika kama Omar Scholarship Fund na tayali watu kadhaa wameshaanza kuchangia.Taarifa za namna ya sifa na uwasilisha wa maombi zitatangazwa baadaye.

Swahili TV itakuwepo katika shughuli za kuuaga mwili ili kukuletea habari za kina na uhakika.

Chanzo: http://swahilitv.blogspot.ca/

--------------------------------------------