Na Godfrey Kahango, Mwananchi
Posted Jumanne,Juni, 2 2015 saa 8:59 AM
Posted Jumanne,Juni, 2 2015 saa 8:59 AM
KWA UFUPI
· Kauli
ya baadhi ya wagombea wa CCM kuwa wameanza safari ya matumia Dk Slaa
anasema inawalaghai Watanzania, kwani wamechoka kuishi kwa matumaini
Tunduma. Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), mwaka huu, unaingia kwenye uchaguzi ukiwa na safari ya uhakika
na siyo ya matumaini kama ilivyotolewa na mmoja wa watangaza nia ya
kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Dk
Slaa alisema, kauli hiyo ni moja kati ya nyingi zinazotolewa na
viongozi wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambazo Watanzania wamechoka
kuzisikia na badala yake wanahitaji vitendo.
Alitoa
kauli hiyo juzi mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, alipokuwa
akihutubia wakazi wa mji huyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika
Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma.
Dk
Slaa alisema Watanzania wanahitaji safari yenye uhakika wa maendeleo
ambayo watayapata Oktoba, mwaka huu, kupitia upinzani lakini siyo
kutoka kwa kiongozi yeyote wa CCM.
“Eti
safari ya matumaini, hivi kweli Tanzania iliyojaa kila aina ya madini
na utajiri wa kutisha halafu tunasema safari ya matumaini badala ya
vitendo? Watanzania tumechoka na kauli za matumaini, tumechoka kuishi
kwa matumaini katika nchi yetu,” alisema Dk Slaa.
Mbali
na hilo, Dk Slaa aliwashangaa baadhi ya watangaza nia wa CCM
walioiponda Serikali yao kwamba imeshindwa wakati wao ndio walitakiwa
kuwa mstari wa mbele kuondoa kero hizo.
Ukawa wajipanga
Akizungumza
kuhusu Ukawa walivyojipanga kuingia Ikulu Oktoba mwaka huu, Dk Slaa
alisema wana akiba ya kutosha ya viongozi makini wa kushika nyadhifa
mbalimbali za uongozi.
Alisema wakishika dola hawatakuwa na sababu yoyote ya kukopa viongozi kutoka kwa CCM.
“Hatuna
njaa ya viongozi ndani ya upinzani, tunao wa kutosha. Hatuna haja ya
kwenda CCM kuwakopa viongozi, Oktoba tupeni ridhaa upinzani tubadili
sura ya nchi,” alisema.
Kwa
upande wake Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde alisema,
licha ya Serikali ya CCM kuamua kugawa majimbo katika maeneo mbalimbali
nchini kwa lengo la kujiokoa, hawataambulia kitu kwani wamejipanga
kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza.
“CCM
tumewagundua na janja yao, baada ya kuona wabunge wao wamekabwa koo,
ndio wanatafuta njia mbadala ya kujiokoa kwa kugawa majimbo, lakini
tunasema majimbo yote yaliyopendekezwa kugawanywa Mbeya kama
yatapitishwa tunachukua yote,” alisema Silinde.
No comments:
Post a Comment