MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA WILAYANI MVOMERO, MOROGORO, TANZANIA
MAADHIMISHO HAYO YALIFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA KIGUGU, KATA YA SUNGAJI, TARAFA YA TURIANI, WILAYANI MVOMERO, MKOANI MOROGORO, TANZANIA TAREHE 16/6/2015.
Na. Zainab M. Mwatawala
Nilialikwa katika maadhimisho haya na Bw. Abdallah Iddi, Muwezeshaji wa Wilaya ya Mvomero, wa Mtandao wa Wakulima Wadogo Wadogo [MVIWATA] kutoa mada juu ya HAKI ZA WATOTO; ambao ndio waliratibu maadhimisho hayo katika kijiji hicho mwaka huu wa 2015.
Taarifa tulizopata kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi KIGUGU Bw. NZINYANGWA MBWAMBO ; ambako ndiko yalikofanyika maadhimisho haya alitoa taarifa ifuatayo juu ya shule yake:
1. Shule ya Msingi Kigugu ilianzishwa mwaka 1975.
2. Hadi sasa ina wanafunzi wa kuanzia shule ya awali hadi darasa la Saba 600
3. Idadi ya Walimu wote waliopo kwa sasa ni 13
4. Shule ina madarasa 8 Tu; wakati mahitaji ya shule ni madarasa 16.
5. Shule ina matundu ya vyoo 6 tu; wakati mahitaji ya shule ni matundu 24.
6. Mwaka jana 2014 wanafunzi 37 walifaulu kuendelea na masomo ya sekondari kutoka idadi ya wanafunzi 61.
7. Shule ina nyumba za walimu mbili [2] tu na walimu wengine wanapanga nyumba za kijijini.
8. Eneo zima la shule ni EKARI 16 wanazotumia kufanya shamba-darasa na nyingine kilimo.
9. Hawana tatizo la maji na umeme kwa kuwa miundombinu yake ipo na inaendelea vizuri.
10. Shule nzima ina madawati 350 tu wanayoyatumia kukaa wanafunzi wawili kila moja.
11. Mwalimu Mkuu alisikitikia madarasa manne [4] yaliyokuwa hayatumiki kutokana na uchakavu, yaliyogeuzwa kuwa kama Bohari ya madawati chakavu na vifaa vingine.
KUHUSU zoezi la uandikishwaji katika Daftari la Wapiga Kura [BIOMETRIC VOTER REGISTER - BVR] lililotakiwa kuanza Kata ya Sungaji tarehe 16/6/2015, mhusika na Uandikishaji wa Daftari hilo alitumia maadhimisho hayo kutangaza kwamba Zoezi hilo katani hapo limesimamishwa hadi siku ya Ijumaa, tarehe 19/6/2015 kwa sababu ya ukosefu wa wino kwa ajili ya zoezi hilo.
Tatizo hilo halikuwakumba kata ya Sungaji pekee. Niliporejea Manispaa ya Morogoro, Muandikishaji Msaidizi wa Kata ya Magadu Moumin Mrisho nae aliniambia kuwa zoezi lilisimamishwa kwa muda kwa kuwa na wao waliishiwa wino. Hata hivyo kwa kuwa kata yao ipo karibu na manispaa ya Morogoro, waliweze kupatiwa wino baada ya kusubiri muda wa saa 3.
Wakati huo huo Bw. Mrisho amenifahamisha kwamba zoezi hilo la kuandikisha daftari hilo kwa kutmia BVR limesimamishwa kutoka tarehe 17/6/2015 hadi tarehe 19/6/2015 ili kupisha shughuli za kukimbiza Mwenge katika Manispaa ya Morogoro.
Kwa maana hiyo, tayari mambo hayo yameshatumia muda mwingi wa zoezi hilo lililopangiwa siku saba kwa kila kata ili kukamilika. Manispaa ya Morogoro ina Kata 29 ambazo zinatakiwa ziandikishe wapiga kura wake; wakati zoezi hilo limeanza rasmi tarehe 16/6/2015.
No comments:
Post a Comment