1.Niko mbele yenu sio kufanya kampeni ya urais, niko mbele yenu kuomba ridhaa ya yenu kugombea nafasi ya urais muda ukifika.
2. Siko hapa kumlaumu mtu au ukimshambulia kwa sababu ukimlaumu mtu umAsikini bado uko palepale. Nikisema historia yangu yote muda hautatosha, kisomo nimesoma mpaka mwisho wa kusoma, kama ni taalumu nimefikia mwisho.
3.Nimepata bahati ya kusoma vyuo vikubwa sana duniani na sehemu kubwa nimepatia Ujerumani ndio maana wengine wanasema nafanya kazi kijerumani.

4. Nimefanya utafiti kwa miaka 30,chama cha majiologia
wamerekani kilichoanza mwaka 1988, mimi niko ngazi ya juu pia kwa
waingereza na wachina niko ngazi ya juu kabisa.
5.Kwenye uasisi mwaka 1976, CCM inaanza 77 sisi ndo
waasisi, kadi hii hapa. Kama nimeweza kutunza kadi ya CCM tangu 75 basi
mimi ndio naweza kutunza rasilimali zenu.
6.Toka tunapata uhuru tuna vikwazo, ujinga, maradhi na umasikini Mwl alitueleza. Nil lazima matatizo yatakuwepo kwenye jamii.
7.Rushwa kubwa na ndogo, ukosefu wa ajira, siasa imekwenda
kila mahala, taifa linanyemelewa na uvuvu na utegemezi, dhulma, upungufu
wa upatikanaji wa takwimu sahihi, tumepungukiwa ushindani kama taifa,
tumeshindwa kujiamini.
8. Haya ndio nataka kuyashughulikia mimi. Upungufu wa mshikamano wa taifa letu. Kwetu asilimia 51 waislamu na 49 wakristo hivyo matatizo ya madhehebu hapa ndipo mahala pake. Afrika ina nchi 54, mimi nimeeenda 52 kasoro Mauritania na Chad. Ningekua sio muaminifu nisingepokelewa huko, ulaya nimezunguka.

9.Lazima Tujue hali halisi ya uchumi wetu, chukueni kalamu
na karatasi. Lazima useme unatoka wapi unaenda wapi! India asilimia 74
wanajua kusoma na kuandika. Nchi inayoongoza kwa watafiti ni
Finland.(Anataja takwimu za nchi ambazo tulikuwa tunafanana uchumi baada
ya vita ya pili ya dunia ikiwemo India, Brazil, China na Kenya.)
Sipendi sana kujilinganisha na Kenya kwa sababu sote ni maskini.
10.Dira ya maendeleo inasema miaka kumi kutoka sasa
Tanzania isiwe nchi masikini, tusikae pembeni, tusogee juu kidogo.
Hakuna mwenye uwezo huo ni mimi tu ili tufikie pato la dola bilioni 200
kutoka dila bilioni 40. Mwaka 2025 tutakuwa milioni 60, nataka tule
miogo na viazi kwa hamu na sio kwa shida.
11.Siwezi kukupa ahadi ya mishahara wakati sijakuza uchumi,
siwezi kukupa ahadi ya kukujengea shule wakati sijakuza uchumi, tukuze
kwanza uchumi.
12.Naombeni ridhaa yenu nisimamishe deni la taifa
lisiongezeke, mwenye dawa ya umaskini ndani ya CCM, CHADEMA, NCCR ni
profesa Muhongo tu. Elimu kuiboresha lazima tuongeze bajeti, haiwezekani
darasa limerundikana ukafundisha. Anaeweza ni mimi tu sababu wengine
utafiti wanausoma kwenye magazeti tu.
13.Wana CCM mnae mwanasayansi wa dunia, si mnipe tu!
Tutatumia rasimali, madini yetu tumeyachimba kwa asilimia 10 kitu, mimi
ndio nimetengeneza ramani ya madini ya Tanzania, Africa na duniani
nikiwa vice president. Nilizunguka hii nchi kuchora ramani ya madini kwa
uzalendo, ningiweza kuja na ramani na kuuzia serikali.
14. Mimi mtu anidanganyi, unakuja tunajadiliana, hii sio
dunia ya kuandikiwa tu, inabidi na wewe ujiandikie. Niliweka mipango ya
kuwapunguzia bei ya umeme. Ilibidi nitoke kidogo mpate machungu
mnichague.
15. Nawaomba ifike mahala ifike mahala tuachane na matumizi ya kuni na mkaa, ni aibu sana. Tutajenga mabomba nchi nzima gesi itumike majumbani. Kila nyumba iwe na mabomba mawili, la maji na la gesi.
15. Nawaomba ifike mahala ifike mahala tuachane na matumizi ya kuni na mkaa, ni aibu sana. Tutajenga mabomba nchi nzima gesi itumike majumbani. Kila nyumba iwe na mabomba mawili, la maji na la gesi.
16.Wengine mnaweza kuwadanganya, mimi hamuwezi
kunidanganya, gesi yenu ipo kwenye mikono ya uhakika kwa professa
Muhongo tangu nimeanza kusoma wakati niko chuo kikuu cha Dar es Salaam
na nimefanya maisha yangu yote.
17.Mapato ya gesi yasiende hazina, tutafungua mfuko maalumu
na bunge litakua linaizinisha asilimia ngapi iende kwenye bajeti.
Mtanzania yoyote asiwe na maamuzi ya kutumia hizo fedha bila idhini ya
watanzania.
18.Mimi sipendi wawekezaji wababaishaji na si kwamba
sipendi wawekezaji wa ndani, haya yote ya ujenzi wa uchumi lazima tuwe
na umeme. Na umeme wa bei nafuu ndio kazi niliyokuwa naianza. Umeme
ulikuwa haukatiki mara kwa mara, muda umefika tusijidharau, lazima
tushinde.
19.Lazima watanzania zaidi ya asilimia zaidi ya 75 wawe
wanatumia umeme, tutatumia vyanzo vyote vya umeme. Lazima mtembee kifua
mbele professa Muhongo amitimiza ahadi ya CCM, hata ilani mpya inayokuja
mtekelezaji atakaetekeleza kwa uhakika ni professa.
20.Ni lazima tupambane na rushwa, na sio maneno kupambana
nazo na nyie wananchi muwe na uelewa na haki zetu. Mnaombwa rushwa kwa
sababu hamjui haki zenu. Naomba ridhaa yenu mniteue niwe mgombea wenu.
Wakulima na wafugani ni mwisho wa kuuana chini ya prof Muhongo, tatizo
sio ardhi, ni technologia.
21.Uwezo ninao, maarifa ninayo, jinsi ya kutafuta fedha ndani na nje, ambacho sina ni nyinyi kuniteua tu.
No comments:
Post a Comment