Dodoma kumekucha, Lowassa nje, matano yajulikana
Kwa ufupiKikao cha Kamati Kuu ya chama cha mapinduzi (CC) kimemalizika hivi punde mjini Dodoma na Katibu wa Itikadi na Ueneze Nape Nnauye ameshindwa kutaja majina matano ambayo yatapelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC)
Saa 1:32 Tovuti ya CCM imeyatangaza majina matano yaliyopitishwa na Kamati ya CCM (CC) kuwa ni Bernard Membe, John Magufuli, Asha-Rose Migiro, January Makamba na Amina S Ali.
Saa 12:55 Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) kimemalizika hivi punde mjini Dodoma na Katibu wa Itikadi na Ueneze Nape Nnauye ameshindwa kutaja majina matano ambayo yatapelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC)
Badala yake amewaambia waandishi wa habari kuwa majina hayo yatatangazwa saa nne asubuhi.
Aidha kwa mujibu wa Matangazo yaliyorushwa moja kwa moja na kituo cha redio Uhuru, Sophia Simba alisikika akisema kuwa mvutano mkali ulikuwemo ndani kikao hicho na wajumbe, Adam Kimbisa, Dk Emmanuel Nchimbi na yeye mwenyewe hawakukubaliana na maamuzi ya kikao yaliyofikiwa.
Saa 10:10 Bado kikao cha Kamati Kuu (CC) kinaendelea taarifa zilizopo ni kwamba kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kimeahirishwa hadi kesho saa nne asubuhi.
Saa 8:12 Kikao cha Kamati Kuu kinarudi kuendelea na kitatoa taarifa ya majina matano ambayo kwa sababu ya muda yatajadiliwa kesho na Kikao cha Halmashauri na Mkutano Mkuu utafanyika kesho mchana, Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Saa 7:00 Kamati Kuu ya CCM imeeenda mapumziko mafupi kwa ajili ya Kufuturu na watarejea tena majira ya saa mbili usiku.
Saa 4:30 KUMEKUCHA Dodoma, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeanza mkutano wake wa Kamati Kuu saa chache zilizopita.
Taarifa kutoka Dodoma zinasema watu wote wameondolewa ndaniya ukumbi mpya wa CCM ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari ambapo hivi sasa wanasubiri taarifa hizo nje ya ukumbi huo.
Endelea kuwa nasi kwa habari zaidi kutoka Dodoma ......Back to Mwananchi: Dodoma kumekucha, Lowassa nje, matano yajulikana.
No comments:
Post a Comment