Imeandikwa nami Zainab M. Mwatawala, 8/7/2015.
HUDUMA MBOVU/OZO ZA KILINIKI ZA WAGONJWA
Tarehe 8/7/2015 mzazi wangu alipangiwa kuanza kiliniki ya Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro. Katika Kadi yake ya Mahudhurio yenye nambari ya Faili lake imeandikwa pamoja na kuhimizwa na Karani wa Hopitali hiyo kwamba mgonjwa anatakiwa afikie hospitalini hapo saa 12.30 ASUBUHI.
Bila kufanya ajizi, niliona ni bora mimi mwenye shida ya mgonjwa niwahi zaidi ya hapo. Mimi nilifika Hospitali saa 12.00 kamili asubuhi, nikitaraji kuwa nitapatiwa matibabu muafaka kama nilivyoagizwa.
Hadi kufika saa 5.00 ASUBUHI, hatujapata huduma yoyote zaidi ya kupewa nambari na kuambiwa tukamsubiri daktari katika chumba kinachohudumia kiliniki husika ya Upasuaji. Fikiri ni kiasi gani cha fedha kilichopotea kwa sote tuliowafikisha wagonjwa wetu hospitalini hapo kwa matibabu ambayo yalicheleweshwa kiasi hicho. Ingekuwa tuko katika shughuli za uzalishaji mali, naamini kwa wauguzaji zaidi ya 30 tuliokuwepo pale tungeweza kuingiza mamilioni ya shilingi badala ya kupoteza muda wetu katika kusubiria huduma ya afya yenye mashaka kiasi kile.
Ilipofika saa tano asubuhi, nikaamua kuulizia matibabu ya FAST TRACK baada ya kukatishwa tamaa na kukalishwa pale bila ya kujua hatima ya wagonjwa pamoja na wa kwangu.
Kwa bahati mbaya siku hiyo, mimi nilimpeleka mgonjwa na wakati huo huo na mimi mwenyewe nilikuwa naumwa, ila kwa upande wangu, nilikuwa na BIMA YA AFYA.
Hivyo wakati tunasubiri kupata huduma kwa mgonjwa wangu, nilifanikiwa kufuatilia mchakato mzima wa BIMA YA AFYA kwa ajili yangu mimi mwenyewe, nikaandikisha, kumwona Daktari na kunihudumia pamoja na kupata dawa NDANI YA NUSU SAA TU. Kutokana na ukweli kwamba nilikuwa nimewahi hospitalini, mimi nilikuwa mtu wa tatu katika foleni ya kwenda kwa Daktari wa BIMA YA AFYA. Na hivyo kuweza kutimitiziwa shida zangu za kiafya mapema kabisa na kurudi kuendelea kusota kusubiria huduma kwa mgonjwa wangu wa KILININI.
Baada ya kuamua kwenda kwenye FAST TRACK, mgonjwa wangu aliweza kuandikiwa X-RAY, na akafanyiwa, akaandikiwa URINALYSIS na akafanyiwa na pia alifanyiwa kipima cha ULTRA SOUND. Dr. MGOA wa hospitali hiyo ndio alimhudumia mgonjwa wangu na kumwandikia vipimo hivyo vilivyogundua ugonjwa wake.
Pamoja na kwamba nililipa zaidi kwa huduma hizo zote, wakati mgonjwa wangu alistahili kutumia HUDUMA BURE kwa kuwa alishapata msamaha wa WAZEE WA ZAIDI YA MIAKA 60, nimeona kwa kuwa AFYA/UHAI wa binadamu hauwezi kupimwa katika mizani ya matumizi ya FEDHA, ninashukuru kwamba ameweza kugunduliwa shida yake na sasa anaendelea na matitabu sawia.
Kwa kweli hizi hospitali zetu tunazoziita ETI NI HOSPITAL ZA RUFAA ni aina ya KEBEHI fulani hivi kwa sababu hazina huduma zifananazo ha HOSPITALI ZA RUFAA kama zitakiwavyo kuwa. Hii ni fedheha sana kuiita HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA halafu wagonjwa wanakaa kusubiri huduma katika muda wa saa 5 bila ya kujua hatima yao.
Tafadhali WIZARA YA AFYA iliangalie jambo hili kwa sababu linawashushia hadhi yao kwa saaaana.
No comments:
Post a Comment