Ufisadi mpya kutikisa
Bunge, asema
Mwenyekiti
wa PAC, Zitto Kabwe
Na Mwandishi
Wetu, Mwananchi
Posted; Jumanne,Januari, 2015 saa 8:9 AM
Posted; Jumanne,Januari, 2015 saa 8:9 AM
KWA UFUPI
·
PAC kusoma ripoti
ya kashfa tatu kubwa kesho Dodoma
·
Jengo la watu
mashuhuri Uwanja wa Ndege ni balaa
·
Misamaha ya kodi,
nyumba ya mbunge kutawala vikao
Dar es Salaam. Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kesho itawasha moto upya bungeni wakati
itakaposoma ripoti maalumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG), ikitarajiwa kuibua kashfa tatu nzito ikiwamo ya misamaha ya kodi.
Kashfa
nyingine zinazotarajiwa kuibuliwa kesho ni, ufisadi katika gharama za ujenzi wa
jengo la watu mashuhuri (VIP) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) na uuzaji wa nyumba ya Bodi ya Korosho.
Habari
zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto
Kabwe zilisema kuwa, tayari kamati hiyo imepokea ripoti ya ukaguzi huo ambayo
inaonyesha ufisadi wa kutisha katika maeneo hayo matatu na mengineyo.
Masuala
hayo matatu pia yaliibuka wakati wa vikao vya kamati za Bunge vilivyomalizika
Dar es Salaam wiki iliyopita, huku bodi ya korosho ikibanwa kuhusu nyumba yake
aliyouziwa Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Silvestry Koka.
Kwa
mujibu wa habari hizo, ripoti hiyo inayoonyesha jinsi ufisadi wa kutisha
ulivyofanywa katika ujenzi wa jengo la (VIP Lounge) na Serikali inadai ilitumia
Sh12 bilioni kulijenga, lakini mthamini wa majengo ya Serikali ameeleza kuwa
jengo hilo lina thamani ya Sh3 bilioni.
Katika
suala la misamaha ya kodi, PAC imepokea taarifa kutoka kwa CAG ikionyesha kuwa
misamaha hiyo iliyokuwa imefikia Sh1.5 trilioni mpaka Juni 2013, lakini baada
ya mwaka moja misamaha hiyo imeongezeka hadi Sh1.8 trilioni mpaka Juni 2014.
“Kwa
mwaka moja tu, misamaha ya kodi imeongezeka kwa zaidi ya Sh300 bilioni. Kiasi
hiki ni kama escrow fulani (Fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow, Sh306 bilioni),”
chanzo cha habari kilidokeza.
Katika
vikao vya kamati hiyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilieleza kuwa misamaha
ya kodi imepanda kutoka Sh1.4 trilioni mwaka 2012/13 hadi Sh1.8 trilioni mwaka
2013/14, chanzo kikiwa ni misamaha ya kodi katika miradi mikubwa. Ilisema kati
ya misamaha hiyo, Sh676 bilioni zinatokana na misamaha ya kodi inayotokana na
Ongezeko la Thamani (VAT) na kuwa hali hiyo itapungua iwapo nchi itaanza
kutumia Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Pia,
TRA ilifafanua kuwa mpaka sasa wafanyabiashara na kampuni kubwa zimefungua kesi
katika mahakama ya rufaa wakipinga kulipa kodi ambayo inafikia Sh1.7 trilioni.
Mvutano
mwingine unaotarajiwa kuibuliwa katika ripoti hiyo ni uwasilishwaji wa utata wa
uuzwaji wa nyumba ya Bodi ya Korosho.
Awali,
hati ya nyumba hiyo ilikuwa ya Taasisi ya Kilimo Tanzania ambayo ilifutwa mwaka
1963, kabla ya mtu mwingine kuibadilisha hati na kuiuza kwa Koka mwaka 2011.
Makamu Mwenyekiti
wa Bodi hiyo, Mudhihir Mudhihir alisema Koka aliuziwa nyumba na taasisi hiyo
ambayo haikuwa mmiliki halali.
Alisema
nyumba hiyo iliuzwa kwa Sh300 milioni na katika juhudi za bodi kufuatilia
taratibu za kuirudisha, ikagundulika kuwa hati imeshabadilishwa, kusisitiza
kuwa uuzwaji wa nyumba hiyo ulifanyika kimakosa bila kufuata sheria na
taratibu.
Juzi
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alikaririwa akiwataka wananchi kutoa
taarifa kuhusu makusudio ya kuuza nyumba za Serikali na mashirika ya umma,
kutokana na madeni mbalimbali ili ziweze kukombolewa kabla ya kuuzwa.
No comments:
Post a Comment