* Kutoka Kagera, Katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wauguzi (Annual General Meeting).
Leo tarehe 30 Sept. 2015
* MADAKTARI, WAUGUZI, WAFAMASIA NCHINI WAUNGA MKONO RASMI VUGUVUGU LA MABADILIKO NCHINI.
Taarifa Maalumu Kwa wadau wa afya nchini (Wataalamu wa afya na wananchi wote). MUHTASARI:
Ndugu
wananchi, na wadau wa afya nchini sisi viongozi wa Jumuiya ya
Madaktari, nchini (MAT), Jumuiya ya Wauguzi nchini (TANNA) Jumuiya ya
Wafamasia nchini (PST), na Association of Medical Practitioner of
Tanzania(AMEPTA) nchini, tumekutana na kujadiliana mambo kadha
yanayohusu mstakabali wa maendeleo mahususi ya sekta ya afya Kama wadau
wa maendeleo,
AJENDA YETU: Afya kuelekea uchaguzi mkuu.
Tumechukua
hatua hii madhubuti Kwa nia njema kabisa tukitambua kuwa sekta ya afya
inakabiliwa na changamoto nyingi na zinahitaji hatua ya dhati kuinusuru
sekta ya afya kuendelea kutoa huduma isiyokidhi viwango, kwani
tunapojadili mstakabali wa afya za watanzania, tunajadili mstakabali wa
harakati za taifa letu kujikwamua kutoka hatua hii ya maendeleo
tuliofikia kwenda hatua nyingine iliyo bora zaidi, Kwa kadiri ya dira ya
maendeleo nchini na duniani kwa ujumla.
* Kwa nini tunachukua hatua hii wakati tuko katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu ifikapo tarehe 25/10/2015,
Jibu:
Ni kwamba tunatambua mustakabali na msingi wa mabadiliko ya kweli
katika sekta ya afya na hata sekta nyingine za umma umo mikononi mwa
Wanasiasa tunaoenda kuwachagua kuanzia madiwani, wabunge na raisi. Hivyo
tungependa(Wahudumu/Wataalamu wa afya na wananchi wote watambue
wanapoamua kuacha kupiga kura, au wanapopiga kura basi wanaamua
mstakabali wa afya yao katika kipindi cha miaka mitano(5) ijayo au
zaidi.
wote
nchini tusifanye makosa, tuamue afya yetu sasa, tuchague kwa makini,
tuchague mabadiliko ya kweli.
Aidha, TUNARIDHISHWA NA TUNAUNGA
MKONO VUGUVUGU LA MABADILIKO NCHINI Kuelekea uchaguzi mkuu ifikapo
tarehe 25/10/2015. "Afya bora Kwa wote inawezekana Tanzania" Tuamue
tarehe 25 Octoba. "Tuchague mabadiliko"
Zipo changamoto zinazoikabili sekta ya afya
1. Uhaba wa dawa na vifaa Tiba:
Hii
inatokana na bajeti finyu ya sekta ya afya, hatuna viwanda vikubwa vya
kuzalisha dawa nchini vinavyomilikiwa na serikali, Tanzania kuna
msambazaji mmoja tu wa dawa nchini, yaani bohari kuu Kwa vituo vyote
nchini huku akiwa hana uwezo wa kutosha kumudu kazi hii muhimu sana. Hii
hufanya Wagonjwa au wateja wa huduma kulazimika kuandikiwa dawa ili
wakajinunulie kwingineko.
Aidha, watalamu wa afya wanalaani na
kuwasihi wanasiasa kuacha mara moja kueneza propaganda kuwa wahudumu wa
afya wanaiba dawa, hivyo kusababisha upungufu wa dawa nchini, wakati
inajulikana wazi upungufu wa dawa unatokana na ufinyu wa bajeti ya
serikali katika sekta ya afya na si vinginevyo, aidha, kauli hiyo
imewasikitasha na kuwapunguzia heshima na morali wa kazi wahudumu wa
afya nchini.
2. Uhaba wa wafanyakazi wataalamu wa afya Kwa
asilimia 56%, yaani chini ya nusu ya hitaji:
Mfano Kwa mwaka 2014,
daktari mmoja alihudumia wagonjwa 20,000(1:20,000) badala ya daktari
mmoja kubudumia wagonjwa 5000(1:5000). Matokeo yake mzigo wa kazi
unakuwa mkubwa na unadhifu wa kazi unapungua.
3: Mazingira magumu
ya kufanya kazi, Miundombinu mibovu,
hadi Leo mwaka 2015 wapo watanzania
wanaolala chini hospitalini, na wengine wanaruhusiwa ikiwa hawajapona
vizuri ili kupisha nafasi Kwa wagonjwa wengine.
Je, watanzania ni kwanini tusitamani mabadiliko?
Mpango wetu;
Nafasi ya wananchi kuelekea uchaguzi mkuu
Sisi
tunatumia fursa hii adhimu kuwakumbusha watanzania wote, kama wadau wa
afya na wadau wa maendeleo wajue wanapopiga kura, au wanapoacha kupiga
kura basi, wanaamua afya zao, wanaamua hatima ya elimu yao, wanaamua
uchumi wao na ustawi wa taifa letu Kwa pamoja. Ni muhimu kila mtanzania
aliyejiandikisha ahakikishe anapiga kura, achague mabadiliko ili
kusaidia kupata viongozi bora watakaosaidia kutatua kero zetu Kwa pamoja
Kama taifa.
Matatizo mengi ndani ya sekta ya afya na hata sekta
nyingine zinaweza kupunguzwa au Kwisha kabisa, tukumbuke baada ya
uchaguzi huduma Kama afya, Elimu na nyingine nyingi hazitolewi Kwa
itikadi ya vyama, tusichague kiongozi kwa mazoea ya chama(chetu),
tuangalie je wanaweza kutusaidia Kama taifa?
Tukifanya makosa
viongozi wasiofaa wakashinda, basi kulala chini hospitalini kutatuathiri
wote, na kutaendelea daima, ilimradi tuko masikini. Ndugu zetu
wanafunzi wakitanzania kukaa chini darasani kutawahusu pia, (tuamue
sasa).
Tunahitaji viongozi wenye kuthubutu, Wenye dira, Maamuzi magumu, na Nguvu ya kusukuma mbele maendeleo yetu Kama taifa.
Dr. P. Magesa
No comments:
Post a Comment