TAMKO HILI LILIKUJA BAADA YA WANA-MTWARA KUANDAMANA KUDAI HAKI YA KUTUMIA WAO GESI YA MTWARA KABLA YA KUNUFAISHA MIKOA MINGINE TANZANIA.
TAMKO LA NDUGU BENJAMIN WILLIAM MKAPA
Katika wiki za hapa karibuni kumekuwa na mijadala na mazungumzo mengi
kuhusu mikakati ya maendeleo ya mikoa ya Kusini hususan Mkoa wa Mtwara.
kuhusu mikakati ya maendeleo ya mikoa ya Kusini hususan Mkoa wa Mtwara.
Mazungumzo hayo yamekuwa na lugha kali na yameambatana, hatimaye, na
maandamano na mikutano ya hadhara. Kiini chake ni matumizi ya gesi
iliyogunduliwa mkoani kwa ajili ya miradi au mipango ya maendeleo ya mkoa
huo, mipango iliyopo mbioni kutekelezwa au inayotarajia kutekelezwa.
Mwenendo wa mazungumzo, maandamano na mikutano ya hadhara imeelekea
kuashiria shari na kuvunjika kwa amani.
Aidha vituko na kauli hizo zimekaribia kujenga kutokuelewana kati ya
Viongozi wa Vyama vya Siasa na Serikali, kati ya wanachama wa vyama vya
siasa na viongozi wao, kati ya wananchi na viongozi wa Serikali. Mtafaruku
huu haufai kuachwa uendeleee na kutishia usalama. Mipango ya maendeleo
siyo Siri. Mikakati na mbinu za Utekelezaji wake siyo Siri. Maelezo yake
mazuri yanaweza kutolewa yakadhihirisha namna na kasi ambayo raslimali
zitawanufaisha wananchi wa eneo zilizomo na Taifa zima. Utekelezaji wa
miradi unategemea masharti kadhaa, k.m. Uwapo wa mitaji na teknolojia.
Lakini pia mwekezaji, awe Serikali au Sekta binafsi, atataka iwepo hali ya
utulivu na usalama wa watu, hali na mali. Hayo yatadaiwa na wawekezaji wa
ndani na wa nje. Vurugu, fujo, vitisho havivutii uwekezaji.
Nikiwa Mwana Mtwara na raia mwema mpenda nchi, nimefadhaishwa sana na
matukio haya ya siku za karibuni Mtwara. Kwa sababu hiyo natoa wito kwa
wadau wote wa maendeleo ya Mtwara kusitisha harakati hizi na maandamano na
mihadhara na badala yake wajipange *KUKAA PAMOJA* katika meza moja, kupitia
historia, kutathmini mipango, kuchambua kwa kina mikakati ya utekelezaji
wake, na hatimaye kufikia muafaka wa Ujia wa maendeleo. Fujo, vitisho,
kupimana nguvu na malumbano kamwe si masharti ya maendeleo. Mazungumzo
yataboresha sera, ya uwekezaji ya mkoa na nchi.
wake, na hatimaye kufikia muafaka wa Ujia wa maendeleo. Fujo, vitisho,
kupimana nguvu na malumbano kamwe si masharti ya maendeleo. Mazungumzo
yataboresha sera, ya uwekezaji ya mkoa na nchi.
Linalowezekana leo lisingoje kesho.
Benjamin William Mkapa
*Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania*
No comments:
Post a Comment