Saturday, August 11, 2012

MOZAMBIQUE AND ZAMBIA AGREE ON COMMON BOARDER

Mozambique and Zambia conclude border demarcation > 2012-08-09 14:33:16.727 GMT > > > Aug. 9, 2012 (Xinhua) -- The Mozambican government said the > conclusion of border demarcation with Zambia will prevent > conflicts between the two nations and in the region as a whole. > The Mozambican Television (TVM) said Thursday that the two > sides have just ended their project to check their common > borders, the work started at the end of last year. > > > Quoting Joaquim Bule, spokesperson for a meeting of the > Mozambique-Zambia joint security commission in Mozambican > capital Maputo since Wednesday, the TVM said one border site has > not been resolved because of difficult access. > > He said it is a mountainous zone and border experts from > the two countries could not be able to realize the work. "It is > a 40 km stretch," he told the TVM. The border stretch already > concluded concerns around 192 km. > > The decision to review the border question was taken after > the Mozambican government discovered that many Zambians were > invading Mozambique to have farms, as well as building homes, > thus abandoning their home country. > > This also happens with Malawians, who are accused of having > fields inside Mozambique. > > Bule said that the remaining border stretch with Zambia > will be dealt with later this year. "It is a continuous work, > which we will also do with other neighboring countries," he > said. > The Mozambican government has already concluded border > demarcation with Tanzania and the Comoros. > > Malawi and Tanzania are in a border dispute at the moment, > because Lilongwe has decided to go ahead with its project of gas > and oil prospection on the Lake Malawi. > > According to the government of Tanzania, the project also > covers the Tanzanian side of the lake. Lilongwe argues that > there is no border line between Malawi and Tanzania on the lake. > > Tanzania is demanding a meeting with the Malawian > government to discuss the matter, the demand was rejected by > Malawi. > > Two days ago, the government of Tanzania threatened that it > was ready for war with its neighbor if Lilongwe goes ahead with > its project, usurping the Tanzanian land. > > Copyright 2012 XINHUA NEWS AGENCY > > -0- Aug/09/2012 14:33 GMT >

Sunday, August 5, 2012

ALIYEMTEKA DR. STEVEN ULIMBOKA HUYU HAPA !!!

Aliyemteka Ulimboka huyu hapa Saed Kubenea's picture Na Saed Kubenea - Imechapwa 25 July 2012 Ni Ighondu wa Usalama wa Taifa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman RAMADHANI Ighondu, afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ndiye ametajwa kuwa mtekelezaji wa mkakati wa utekaji wa Dk. Steven Ulimboka, MwanaHALISI limegundua. Afisa huyo, licha ya kutambuliwa na Dk. Ulimboka mwenyewe, ndiye simu yake ilitumika kuandaa kikao ambako daktari alitekwa. Ni afisa huyohuyo wa usalama ambaye alikutana na Dk. Ulimboka dakika chache kabla ya kutekwa. Uchunguzi umegundua kuwa Ramadhani Ighondu (34), ni mfanyakazi wa ikulu aliyekuwa akifanya mawasiliano ya mara kwa mara na Dk. Ulimboka. Ni mfanyakazi huyuhuyu ambaye Dk. Ulimboka amenukuliwa akisema, “...alinipigia simu na kuniita kwenye kikao ambako muda mfupi baadaye nilitekwa.” Nyaraka nyeti ambazo mwandishi ameona zinaonyesha kuwa Ramadhani ndiye pia huitwa “Rama” – jina ambalo hutumia katika kujitambulisha na katika baadhi ya mawasiliano. Rekodi katika simu ya Dk. Ulimboka: Na. 0713731610 zinaonyesha Rama ndiye alifanya mawasiliano ya mwisho na daktari huyo muda mfupi kabla ya kutekwa. Aidha, ni Rama ambaye alikutana na kiongozi huyo wa Jumuia ya Madaktari Tanzania, maeneo ya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya kutekwa. Dk. Ulimboka alitekwa usiku wa 26 Juni, kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno; na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande. Rama alifanya mawasiliano ya mwisho na Dk. Ulimboka saa 5: 52 kupitia simu yake Na. 0713 760473. Dokta alitekwa “muda mfupi” baadaye. Rais Jakaya Kikwete aliliambia taifa kwa njia ya televisheni, mwishoni mwa Juni, kuwa serikali yake haihusiki na kuteka, kutesa na kutupa daktari porini. Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia bunge kuwa serikali yake haihusiki na utekaji na utesaji; na kuuliza, “...serikali imteke ili iweje?” Mawasiliano katika simu ya Dk. Ulimboka yanaonyesha mtiririko wa simu za Rama wa ikulu hadi muda wa kutekwa katika eneo la Leaders Club. Vyanzo vya taarifa ndani ya idara ya usalama wa taifa vinasema, kwa sasa Rama “amehifadhiwa” kwenye jengo moja la kificho linalotumiwa na idara hiyo lililopo eneo la Ada Estate, Kinondoni, Dar es Salaam. MwanaHALISI limeweza kuthibitisha, kupitia vyanzo vya taarifa na nyaraka mbalimbali kuwa, simu Na. 0713 760473 iliyokuwa ikifanya mawasiliano ya mara kwa mara na Dk. Ulimboka, ni mali ya Rama. Huyo ndiye Ramamadhani Ighondu (Rama). Mzaliwa wa Makole, Dodoma. Mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Idara hii iko chini ya Ofisi ya Rais (Utawala Bora) inayoongozwa na Rashid Othman. Gazeti hili limepitia nyaraka mbalimbali, likiwamo daftari la kudumu la wapigakura lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kupata fununu zaidi juu ya tuhuma za Dk. Ulimboka kwa Rama. Katika daftari hilo ambalo limetumika kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Rama anaonekana kujitambulisha kama ifuatavyo: Ramadhani Ighondu, Nickname: Rama Born: 28.08.1978 Place: Makole – Dodoma Voter Registration Card: 49406879 Mobile Number: 0713 760473 Dk. Ulimboka ambaye anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini, amethibitishia MwanaHALISI kuwa mtu ambaye alikuwa anawasiliana naye mara kwa mara na kumuita kwenye mkutano maeneo ya Leaders Club, 26 Juni 2012, anatumia simu Na. 0713 760473. Akizungumza kwa kujiamini Dk. Ulimboka amesema, “Ndiyo. Hiyo namba naikumbuka vizuri. Ni 0713 760473. Mwenye namba hiyo alikuwa akijitambulisha kwangu kwa jina la Abeid. Huyo bwana ndiye niliyekutana naye Leaders Club muda mfupi kabla ya kutekwa.” Alipoulizwa anawezaje kukumbuka namba iliyokuwa inafanya mawasiliano na yeye wakati kipigo alichokipata kutoka kwa watekaji kilikuwa kikubwa hadi kupoteza fahamu, Dk. Ulimboka alisema: “Ninafahamu ninachokisema. Huyo bwana nilikuwa ninawasiliana naye mara nyingi na niliwahi kukuta naye katika mgogoro ule wa kwanza wa madaktari.” Kauli hii ya Dk. Ulimboka inafanana na ile aliyoitoa kabla ya kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, 30 Juni 2012. Katika mahojiano yake yanayopatikana kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, Dk. Ulimboka anasema, “Huyu bwana kwa muda wa siku tatu mfululizo alikuwa anajaribu kuwasiliana na mimi lakini kwa bahati mbaya ratiba yangu ilikuwa haiwezekani kumuona. “Nilishawahi kukutana naye kwenye mgogoro ule mwingine, lakini this time of course (mara hii) alikuwa serious (makini) akinitafuta…Huyu bwana anafanyakazi ikulu.” Katika mahojiano hayo, Dk. Ulimboka anasisitiza kuwa wakati anatekwa alikuwa na akili timamu na hivyo anamfahamu aliyemteka kuwa ni mtu kutoka ikulu. Dk. Ulimboka anasimulia “mtu wa ikulu” alivyoingia kwa gari pale walikomwambia wameketi na kumuuliza iwapo alikuwa na Deo (Dk. Deogratias Michael) na kwamba walianza majadiliano yaliyohusu hali ya mgomo na jinsi wao walivyokuwa wakiona unaweza kutatuliwa. “Sisi tukasema mambo yote yanafahamika. Tukaongea naye kwa muda mfupi tu; akawa anaandika… kwa hiyo pia alikuwa very busy communicating, (akionekana kujishughulisha zaidi na mawasiliano ya simu). Unaona?” MwanaHALISI limegundua kabla ya Dk. Ulimboka kutekwa, Rama alianza kufanya mawasiliano naye saa 12: 25 jioni. Mawasiliano hayo yaliendelea 3:29 usiku, saa 4: 52, saa 5: 27, saa 5:40 na mwisho ilikuwa saa 5:52 usiku. Haya ndiyo mawasiliano ambayo Dk. Ulimboka aliishasimulia kuwa yalielekea katika kukutana kwake na mwenye simu Na. 0713 760473. Ni mwenye simu hii aliyeandaa mkutano, anakumbuka Dk. Ulimboka. Kabla simu ya Rama kumwita Dk. Ulimboka kwa mara ya kwanza siku hiyo, saa 12:25, ilifanya mawasiliano na Buruani Ntilongwa, mmiliki wa simu Na. 0712 359533. Mawasiliano hayo yalifanyika kati ya saa 2: 08 na 2: 24 usiku. Aidha, nyaraka zinaonyesha kila pale Rama alipowasiliana na Dk. Ulimboka, alifanya mawasiliano pia na Moshi Marungu Shabani anayemiliki simu Na. 0761 132663 na 0655 162663. “Nakwambia ndugu yangu, kila pale ambapo Rama alifanya mawasiliano na Dk. Ulimboka, utaona hapohapo alifanya mawasiliano na Abdallah Kunja na Ntilongwa. Hawa ni watu muhimu sana kwenye sakata hili,” taarifa zimeeleza. MwanaHALISI limegundua kuwa siku mbili kabla ya Dk. Ulimboka kufanyiwa unyama huo (24 Juni 2012), simu ya Rama iliingizwa salio la Sh. 252,849. Hili ni salio kubwa pekee kuingizwa kwenye simu hiyo tangu mwanzo wa mwaka huu. Nyaraka zinaonyesha tarehe 4 Mei 2012 simu ya Rama iliwahi kuishiwa salio kabisa hadi kufikia kiwango cha Sh. 1. Kwa mujibu wa nyaraka hizo zilizosambazwa na kituo cha sheria na haki za binadamu sehemu mbalimbali duniani, Rama kila alipomaliza kumuita Dk. Ulimboka, haraka alipiga simu kwa Kunja, Ntilongwa na Marungu. Wengine ambao walikuwa na mawasilino ya mara kwa mara na Rama kabla ya kutekwa kwa Dk. Ulimboka ni: Mohammed Hassan Na. 0655 524444 Shomari Kondo Na. 0714 666304 Optat Jacob Marandu Na. 0716 611625 Mbega Hisbert Na. 0715 222778. Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo kwenye daftari la wapigakura la NEC, Mohammed Hassan, ni mkazi wa Ilala, Dar es Salaam. Amezaliwa 12 Agosti 1980. Mbali na kumiliki namba hiyo, anatumia pia namba nyingine: 0717 242789. Naye Shomari Kondo amezaliwa 1 Januari 1976. Ni mkazi wa Dar es Salaam. Anamiliki simu nyingine Na. 713 671640. Marandu ametambuliwa kwenye daftari hilo kuwa amezaliwa 1979 mkoani Dodoma; huku Mbega akionyeshwa kuzaliwa 16 Mei 1978 na mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam. Taarifa nyingine kutoka ndani ya idara ya usalama wa taifa zinasema, tangu 26 Juni 2012, pale jaribio la kumteka Dk. Ulimboka lilipofanikiwa, Rama aliacha kutumia simu yake hiyo. Alianza kutumia tena simu yake, tarehe 1 Julai kwa kutuma ujumbe mfupi (sms). Namba alizokuwa anatumia sana kuwasiliana kuanzia 1 Julai 2012 ni: 0714 293425 0717 030405 0713 510585 na 0715 466995. Toleo lililopita la gazeti hili lilimnukuu mtoa taarifa akisema, “Wakati wakimtesa Ulimboka, ni Rama aliyekuwa akisisitiza kuelezwa kama Ulimboka ametumwa na CHADEMA na kwamba ni nani hasa katika CHADEMA anayemtumia.” Mmoja wa watoa taarifa wa ndani ya idara ya usalama anasema, “Wazo lililopo Usalama wa Taifa ni kuwa Ulimboka anatumiwa na Mnyika pamoja na Dk. Slaa.” Wengine ambao ni maswahiba wa Rama aliowasiliana nao mara nyingi katika kipindi hicho ni: Abdi Abdi Na. 0713 229919 Najma Damian Na. 0712 704908 Spa Wilson I. Sima Na. 0712 540502 na Zulfa Swalehe Na. 0719 496505. Katika daftari la wapigakura, Abdi Abdi anaonyesha amezaliwa 1977; Spa Wilson I. Sima amezaliwa mwaka 1960 na Zulfa Swalehe amezaliwa mwaka 1950. Rama ni mfanyakazi wa idara ya usalama wa taifa aliyepo chini ya naibu mkurugenzi wa idara ya usalama anayeshughulikia siasa, Jack Zoka. Anadaiwa kushiriki kikamilifu kumtesa Dk. Ulimboka katika moja ya majumba ya kificho na hatimaye kumtelekeza msituni Mabwepande, nje ya jiji la Dar es Salaam. Uchunguzi huu unakuja baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Zoka, ndiye mtuhumiwa Na. 1 kwenye sakata la utekaji na utesaji wa Dk. Ulimboka. Zoka anatajwa pia katika kilichoitwa “…njama za kutaka kuangamiza” maisha ya katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, mbunge wa Ubungo, John Mnyika na wengine waliopachikwa jina la “wakosoaji wakuu wa serikali.” Taarifa mpya za uchunguzi juu ya maandalizi na kutekwa kwa Dk. Ulimboka, zinakuja wiki moja tangu Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi mkoani Dar es Salaam, Suleiman Kova atangaze kufikisha mahakamani mtu mmoja aliyedai amekiri kuhusika na utekaji wa Dk. Ulimboka. Kova aliwaambia wandishi wa habari kuwa polisi wamekamata mtu aitwaye Joshua Malundi kutoka Kenya ambaye amekiri kuteka na kutesa Dk. Ulimboka. Amedai kuwa mtuhumiwa alikwenda kutubu katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe, Dar es Salaam. Lakini tayari mchungaji wa kanisa hilo, Josephat Gwajima amekana kauli ya Kova juu mtuhumiwa wake na kusema, “Serikali lazima ieleze vizuri.” Mchungaji Gwajima amewaambia waamini wake, “Kwanza huyo mtu hajaja kwetu kutubu...kama kutubu, basi mtu huyo angetubu huko kwao Kenya na kuhoji, “…kwani kwao Kenya hakuna Mungu?” Taarifa za kuaminika zinasema, polisi hawajawahi kuwahoji Dk. Deogratias Michael aliyeshuhudia Dk. Ulimboka akitekwa; Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) Hellen Kijo-Bisimba wala Onesmo ole Ngurumwa, mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini waliokwenda kumchukua polisi Bunju. Gazeti toleo lenye makala hii

RUSHWA YAVURUGA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA !

RAIA MWEMA On Aug 2, 2012 Rushwa yavuruga Bunge Mwandishi Wetu Toleo la 252 1 Aug 2012 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe BAADA ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu wake Mkuu, Eliakim Maswi, kunusurika kung’olewa na mtandao wa mafisadi kupitia kwa wabunge wanaodaiwa kupewa rushwa kutimiza azma hiyo, taarifa zinaeleza zamu inayokuja ni dhidi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Membe anatarajiwa kuwasilisha hotuba yake bungeni wiki ijayo, na inaelezwa kwamba msimamo wake dhidi ya watuhumiwa wa kashfa ya ununuzi wa rada umemfanya kusubiriwa kwa hamu na baadhi ya wabunge ambao nao wanaelekezewa tuhuma kupewa fedha na mafisadi ili kushinikiza kumng’oa waziri huyo au hata kumchafua wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara yake. Maandalizi hayo dhidi ya Waziri Membe yanakuja katika wakati ambao, vyanzo kadhaa vya habari vya gazeti hili vinamnukuu Rais Jakaya Kikwete akipata kumweleza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba; “nimechoka kuapisha mawaziri wapya,” akiwa na maana hataki kumpoteza waziri yeyote kwa sasa. Kikwete anakaririwa kutoa kauli hiyo baada ya joto la mafisadi kupitia wabunge kutaka kumng’oa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter na Katibu wake, Maswi ambao wanaaminika kudhibiti mirija ya unyonyaji ya mafisadi iliyopachikwa katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Mpambano uzalendo vs ufisadi Katika harakati za kuokoa jahazi na kudhibiti nguvu ya mafisadi katika kuwang’oa viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, baadhi ya mawaziri, wabunge na timu nyingine maalumu zilizoshirikisha viongozi kutoka makao makuu ya CCM, zilishiriki huku baadhi ya wabunge wa kambi ya upinzani wakiunga mkono juhudi hizo katika imani ya kupigania maslahi ya Taifa. Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa stahili iliyokuwa ikitumiwa ni kupita kila walipokuwa wakipita ‘mawakala’ wa ufisadi ambao nao walikuwa wakiwaona wabunge mmoja mmoja kwa kuzingatia orodha waliyojiandalia. Katika juhudi hizo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, anadaiwa kulazimika kutumia usafiri wa bajaji nyakati za usiku kupita kwa baadhi ya wabunge ili kuwaeleza hali halisi ni kwa nini viongozi wapya wa Wizara ya Nishati na Madini wanapigwa vita. Mbali na Waziri Kabaka, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, naye alikuwa na kazi maalumu ya kupita kila alipokuwa akipita mbunge mmoja kutoka moja ya majimbo mkoani Arusha (CCM). Inadaiwa kuwa mbunge huyo alikuwa na kazi ya kusambaza fedha ili ‘kuwanunua’ wabunge wafanye mashambulizi dhidi ya uongozi wa wizara, fedha ambazo alizipata kutoka kwa baadhi ya kampuni zilizowahi kufanya biashara na TANESCO kwa njia za kifisadi. “Kazi ilikuwa moja tu, wao wanapoondoka katika ‘kijiwe’ fulani baada ya kugawa fedha sisi tulikuwa tunakwenda kueleza ukweli na kwa kulinda maslahi ya nchi badala ya maslahi ya genge la wafanyabiashara wanaotafuna nchi,” alieleza mtoa habari wetu. Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Kangi Lugola naye anadaiwa kutembea kilomita kadhaa bila usafiri wa chombo chochote, akitoka hoteli moja kwenda nyingine ili kuweka mambo sawa kwa kufichua ukweli kwa wale waliopewa rushwa. “Kazi ilikuwa moja tu ambayo ni rahisi. Ilikuwa ni kazi ya kusema ukweli, kwa maslahi ya nchi. Tulikuwa tunasema fedha za rushwa zimetoka kwa nani, kwa sababu gani na kwa maslahi ya nani na kwa malengo gani hasa dhidi ya nchi,” alieleza mtoa habari wetu. Waziri Mkuu na Rais Kikwete Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa siku chache kabla ya joto la mafisadi kupanda na kuelekea kutaka kufanikiwa, Rais Kikwete anatajwa kumwita Waziri Mkuu na kumweleza kuwa amechoka kuapisha mawaziri wapya. Kauli hiyo ni kama ilikuwa agizo kwa Waziri Mkuu ambaye kichwani mwake alikuwa na kumbukumbu ya shinikizo la wabunge lililosababisha kusukwa upya kwa Baraza la Mawaziri. Baada ya hapo, Pinda aliitisha kikao cha wabunge wa CCM walioko katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. Wengine waliokuwamo katika kikao hicho ni pamoja na Spika wa Bunge, Anne Makinda, Waziri Profesa Muhongo na Katibu Mkuu, Maswi. “Kikao kilidumu kwa saa sita hivi. Hali ilikuwa tete na Katibu Mkuu aliwaumbua baadhi ya wabunge. Aliwataja kwa majina wanaonufaika na TANESCO ambao ndio hao waliokuwa wakitetea viongozi waliosimamishwa kazi TANESCO warejeshwe. “Wabunge wawili wa Viti Maalumu walirushiana matusi pale. Mmoja alimwambia mwenzake anatetea ufisadi wa TANESCO kwa kuwa anafanya biashara na shirika hilo, naye alisimama kumjibu bora yeye anafanya biashara na TANESCO kuliko mwenzake huyo anayefanya biashara kwa kuuza mwili wake. “Maswi pia alimkumbusha mbunge mmoja namna alivyowahi kwenda kumwomba rushwa ya shilingi milioni 50 ili aende akawagawie wenzake. Alipomwambia hana kiasi hicho cha fedha alipunguza dau hilo hadi shilingi milioni 20. Ushahidi wa hilo umehifadhiwa na utawasilishwa sehemu husika,” kinaeleza chanzo chetu cha habari. Malecela aitwa kuokoa jahazi Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela, alilazimika kutumika pia. Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatajwa kumwomba amweleze hali halisi mbunge mmoja kutoka mkoani Arusha ili aache kuendelea kuwa wakala wa mtandao wa mafisadi waliokuwa wakinufaika na TANESCO. “Mzee Malecela alikaa na .... mbunge (jina linatajwa) akamweleza kila jambo lakini jamaa alikuwa kichwa ngumu. Mzee alimwambia unakwenda kujimaliza kisiasa siku si nyingi, yeye akaendelea na msimamo wake, kwa hiyo Mzee akamwacha na sasa hali yake kisiasa ni mbaya. Yeye ni sehemu ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa,” kinaeleza chanzo chetu cha habari. Siri ya wabunge kuomba rushwa Siri za baadhi ya wabunge wa Bunge na hasa katika kuomba na kupokea rushwa nazo zimezidi kuanikwa na baadhi yao, wakilielezaRaia Mwema kwamba, wengi waliochukua mikopo ya hadi shilingi milioni 200 na kuanzisha biashara, biashara hizo zimekufa na mshahara wao ‘unatumikia’ mikopo hiyo na kwa hiyo, hawana chanzo kingine cha mapato. Kutokana na hali hiyo, wabunge wamekuwa wakililia nyongeza ya mishahara na posho na kwa kupitia kamati zao wengine wanadai hufanya shinikizo la kupewa semina na baadhi ya mashirika na taasisi za umma. Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa gazetini wamesema mbali na wabunge kuwa katika hali hiyo ngumu, kuna udhaifu wa serikali kiasi cha kuacha wabunge kuingilia shughuli za kiutendaji za kiserikali. “Kutokana na serikali kama mhimili wa dola kuonekana kuzidiwa na Bunge na hivyo kuwa too submissive to the parliament(kujisalimisha kwa Bunge), Bunge limejikuta likitumia vibaya nafasi yake ya kuisimamia na kuishauri serikali kwa kujiingiza kwenye masuala madogo madogo ya utawala na utendaji wa siku hadi siku. “Wameacha kuisimamia serikali katika masuala ya kisera, sasa wanakuwa mawakala wa wafanyabiashara waliokosa zabuni au wafanyabiashara wanaofutiwa leseni,” anaeleza mmoja wa wabunge kutoka Kanda ya Ziwa. Katika kuongeza nguvu hoja hiyo, mbunge mwingine anasema; “Wanaolalamika kuonewa au vyovyote wanapaswa kwenda mahakamani na si kwa wabunge, tena kwa kuwapa fedha. “Wafanyabiashara wengi wanaoathirika na uamuzi wa watendaji wa serikali, siku hizi hawaendi tena kortini kupinga uonevu wanaodhani wamefanyiwa, wanakimbilia bungeni kwa wabunge.” Mbunge mwingine kutoka Nyanda za Juu Kusini anataja sababu nyingine za wabunge kudai rushwa ni mfumo wa uchaguzi wa wabunge ambao ni wa gharama kubwa na baada ya uchaguzi, wananchi waliosaidia kampeni za mbunge wamekuwa wakiwageuza wabunge kama vyanzo vya mapato yao. Anasema wabunge pia huchukua mkopo na kuanzisha biashara ili kujiongezea kipato lakini wengi kwa kukosa utaalamu wa biashara, biashara hizo zimekufa na wakati huo huo, mishahara yao ikikatwa kwa sehemu kubwa kufidia mkopo. ‘Kamati Maliasili ivunjwe’ Baada ya wito wa kutaka kamati za Hesabu ya Mashirika ya Umma inayoongozwa na Kabwe Zitto, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa inayoogozwa na Augustine Mrema na Serikali Kuu ya John Cheyo zivunjwe, kama ile ya Nishati na Madini kutokana na tuhuma mbalimbali za ufisadi, wito umetolewa sasa kwa Spika Makinda kuvunja kamati nyingine za Bunge. Kamati hizo ni pamoja na Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Kamati ya Uchumi na Fedha na Kamati ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje. Kamati za Ulinzi na ile ya Uchumi na Fedha zinashinikizwa na baadhi ya wabunge zivunjwe kwa kuwa wenyeviti wa kamati hizo tayari uadilifu wao unatiliwa shaka mbele ya wananchi. Kamati hizo zinaongozwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na ile ya Uchumi inaongozwa na Andrew Chenge. Lowassa alijiuzulu baada ya shinikizo kutoka katika Bunge la Tisa akihusishwa na kashfa ya kampuni tata ya ufuaji umeme ya Richmond. Chenge anatazamwa kama kiongozi aliyefanikisha ununuzi wenye utata wa rada ambayo mchakato wake ulitikisa mapaka kwenye bunge la Uingereza. Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwa Lowassa na Chenge, Kamati ya Ardhi inayoongozwa na Mbunge wa Kahama, James Lembeli, inadaiwa kutiwa mfukoni na genge la wafanyabiashara, ikidaiwa kwamba kwa nyakati tofauti genge hilo limewahi kuwalipa posho wajumbe wa kamati hiyo ili kujadili uamuzi wa serikali wa kuzuia vibali vya usafirishaji wanyama nje ya nchi. Kamati hiyo ya Lembeli ‘ilitiwa mfukoni’ na wafanyabiashara hao katika kikao kilichofanyika Siku ya Jumapili (Novemba 6, 2011), siku ambayo si siku ya kazi za Bunge na inadaiwa wajumbe walilipwa na wafanyabiashara hao. Semina hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa, bungeni mjini Dodoma. Kamati hiyo pia inadaiwa kuwahi kulipiwa ukumbi wa semina na posho kwa wajumbe wake na wafanyabiashara wa uwindaji wa kitalii, semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Mtakatifu Gaspar, mjini Dodoma, Aprili, mwaka huu. Chazno: Gazeti la RaiaMwema

THE TANZANIA BUNGE CREDIBILITY QUESTIONED

The Citizen Reporter, Sunday, 05 August 2012 01:44 Dar es Salaam. Corruption allegations, absenteeism and flagrant disregard for rules governing parliamentary procedures have eroded the National Assembly’s credibility to an extent that warrants the House’s dissolution, according to some observers. This view comes in the wake of revelations that many MPs have been receiving bribes from lobby groups and companies in return for business or policy favours However, Deputy Speaker Job Ndugai dismissed calls for Parliament’s dissolution, saying recent tumultuous events in the House were a sign of growing transparency. Political analysts and observers who spoke to The Citizen on Sunday said developments in Parliament were gradually eroding Tanzanians’ trust in the country’s main oversight body. Those who called for its dissolution include the Executive Director of the Legal and Human Rights Centre (LHRC), Dr Helen Kijo-Bisimba, who said Parliament’s dignity had been greatly compromised. “It is a big shame that an entity that is supposed to safeguard the interests of ordinary Tanzanians has turned against the very people it is meant to help. Do we have anything to trust as far as checking the government’s excesses is concerned?” she asked. Dr Kijo-Bisimba said the bribery allegations were hardly surprising because many MPs bribed their way to Parliament, adding that the claims were a reflection of the failure of the National Electoral Commission (NEC), political parties and anti-corruption watchdogs. She said LHRC was pushing for inclusion in the new constitution of a provision that would allow voters to reject MPs who lose credibility. Asked how sure she was that clean MPs would be voted in after Parliament’s dissolution, Dr Kijo-Bisimba said: “I don’t believe we Tanzanians cannot choose credible parliamentarians.” However, Deputy Speaker Job Ndugai said dissolving the House was counterproductive, adding that the enormous cost of electing a new parliament must be taken into consideration. “The House has more than 350 members and corruption allegations have been levelled against a few MPs. Parliament should be praised for high levels of transparency. This is why these allegations were raised in the first place. Had we decided to protect those being accused, who would have known the allegations?” he asked. Mr Ndugai said MPs’ conduct was a reflection of moral decadence in society. “We in Dodoma just receive MPs from the constituencies. These people are employed by voters. We cannot be part of the problem if the people bring to us crooked individuals as their representatives.” Dr Cosmas Kamugisha of the University of Dar es Salaam’s Institute of Development Studies said what was happening in Parliament was a sign of greater democracy and transparency. “These things did not start today. They have been there for a long time but were not being exposed due to lack of transparency and good governance,” he said. Dr Kamugisha said there was a need to take an institutional rather than individual approach in addressing corruption among MPs. “Let’s not look at individual MPs. We will fail to tackle the sourc'e of the problem. The issue is not corruption, but the source of corruption and institutions charged with taming the vice. If we dissolve the House, how sure are we that the next MPs will be clean?” he asked. Two weeks ago Parliament failed to approve Ministry of Agriculture, Food Security and Cooperatives’ 2012/13 budget for lack of quorum. The situation prompted the Speaker, Ms Anne Makinda, to voice her concern about absenteeism and warned that MPs would be required to seek permission before travelling outside Dodoma. The arraignment of Bahi MP Omar Badwel on charges of soliciting and receiving a Sh1million bribe from a district executive officer so that the district council’s report could be approved is among recent developments that have tarnished Parliament’s image. Things came to a head when Energy and Minerals minister Sospeter Muhongo told the House that some MPs had been bribed to frustrate efforts to unearth grand corruption in Tanzania Electric Supply Company (Tanesco). This led to the dissolution of the Energy and Minerals Committee and appointment of a five-member committee to investigate the allegations. Civic United Front (CUF) chairman Ibrahim Lipumba said the allegations did not amount to a national crisis to warrant Parliament’s dissolution, but added the claims showed that MPs were not taking their jobs seriously. “Many are business-minded and do not put the interests of their voters first,” he said. He proposed the formation of an independent committee led by a judge to investigate the allegations instead of entrusting MPs with the task. In June, last year, Kigoma South MP David Kafulila named three MPs in the Local Authority Accounts Committee, whom he claimed were receiving bribes, but he was cut short and told to wait for guidance on the matter. No action was taken. A year later, Mr Badwel was arraigned on corruption charges. “Inaction on the part of the Speaker caused these things to continue. It is very unfortunate that one of the MPs I named was arrested for corruption,” Mr Kafulila said.

STEVEN WASSIRA NA UWAZIRI WA MAHUSIANO NA URATIBU (MWANAMASUMBWI T Y S O N)

Wassira unafaa kuwa Waziri wa Mahusiano? Na Ratifa Baranyikwa Source “Tanzania Daima”, Tanzania: 16 Juni, 2012) WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira, wadhifa anaouvaa hauendani na mwenendo pamoja na utendaji wake. Yasemekana lengo kuu la wizara anayoiongoza, ni kushughulikia mahusiano kwa maana ya kuhakikisha migogoro inayojitokeza kwenye jamii inadhibitiwa. Kwa bahati mbaya sana, kiongozi kama Wassira aliyepewa wizara inayoshughulikia mahusiano, sijui kama anafahamu kwamba anapaswa kutambua mafanikio binafsi na yale ya kitaaluma, ukichanganya pia na malengo ya wizara yanayotegemea mahusiano mazuri kati yake na wale anaowaongoza. Nitaangazia matukio machache tu kati ya mengi ambayo yanamvua Wassira sifa ya kutofaa katika wadhifa wa wizara aliyopewa. Kwanza, ni hasira ambazo amekuwa akishindwa kuzidhibiti wakati anapokuwa akijibu maswali, hata yale ya kukera. Kwa mfano, hivi karibuni alipozomewa na wananchi wa jimbo lake la Bunda, kiongozi huyu alishindwa kujibu vizuri maswali aliyoulizwa na wananchi wake, na badala yake aliruhusu hasira. Maswali ya wananchi hao ni pamoja na lile la kumtaka aeleze ni kwa nini eneo la Shule ya Msingi Balili limechukuliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya, Chiku Galawa, ambaye sasa ni mkuu wa mkoa wa Tanga, na wananchi walishalalamika, lakini yeye hajawahi kulizungumzia. Katika majibu yake, Wassira alijibu swali hilo kwa mkato kuwa hawezi kulisemea hilo, kwamba ni la watu wa ardhi. Inawezekana kabisa Wassira akawa sahihi katika majibu yake hayo, na pia asiwe sahihi kwa upande mwingine, hoja nitajenga baadae. Swali jingine ambalo linamvua sifa Wassira katika Wizara ya Mahusiano, ni pale alipoulizwa kuwa, katika mkutano huo alikuwa anahutubia kama mbunge, waziri au kada wa CCM, kwani alitakiwa kufahamu kuwa Bunda ina wanachama wa vyama vingi. Lakini katika majibu yake, alihoji kwa ukali: “Kwani Wenje (Mbunge wa Jimbo la Nyamagana-CHADEMA) alikuja kuhutubia hapa hivi karibuni kama nani?” Na hapo ndipo tunaelezwa kuwa wananchi walianza kumzomea. Mfano mwingine ni huu wa juzi, ambako Waislamu wametangaza kuisusia sensa na sababu wanayoitoa ni kutoridhishwa na majibu ya Wassira, kadhalika ubabe aliowaonesha. Inawezekana kabisa ndugu zangu Waislamu hoja zao zikawa si za msingi, lakini katika kujibiwa, kuna mambo ambayo Wassira alitakiwa kuyaangalia kwa makini. Kwa mifano hiyo michache, namuona Wassira amekosa sifa muhimu zifuatazo: 1. Kwa mfano nikianza na swali aliloulizwa kuhusu ardhi, ni kweli jambo hilo linawahusu watu wa ardhi, lakini yeye kama kiongozi na mwakilishi wao, alisahau jambo moja kubwa la wajibu. Pengine kwa majibu rahisi alipaswa kulisemea hili. 2. Jambo la pili, ambalo linamgusa Wassira ni hili la kutosikiliza na kuchukua muda wa kutafakari kujibu hoja kwa kuangalia aina ya watu anaowajibu, badala yake amekuwa akitumia hasira zaidi. 3. Tatu, anatumia nguvu kubwa kusukuma hoja zilikotoka na kujitetea hata katika hali ambayo hana hoja ya kujitetea. Kiongozi huyu namuona ni mtu wa kukosa uvumilivu, anashindwa kufahamu umuhimu wa kukumbuka kwamba hata kama kile watu wanachokisema ni ukweli kwao, haijalishi ni jinsi gani atajisikia. 4. Nne, Wassira anashindwa kutambua kwamba kazi yake ya mahusiano kuna kitu kinaitwa msamaha. Katika somo zima la mahusiano ya kikazi, inaelezwa bayana kuwa; omba msamaha pale inapotakiwa. Kama kile wanachokisema ni sahihi na umekosa, omba msamaha. Katika hili, narejea mfano wa Waislamu ambao wanadai kuwa katika vikao walivyokutana na Wassira kuna wakati alichelewa, na pia kuwatolea majibu waliyoyaita kuwa ni ya kibabe. 5. Tano na mwisho, Wassira si mtu wa kumshukuru mtu anayeongea kwa uwazi na ukweli, na hivyo suala la mahusiano kwake kumpa wakati mgumu. Namshauri Wassira apime hayo juu.

MWALIMU AFUKUZWA KAZI TANZANIA KWA KUZUNGUMZA LUGHA YA TAIFA !!!!

ATI, MWALIMU AFUKUZWA KAZI KWA KUZUNGUMZA KISWAHILI !!!!! FEDHEHA GANI HII KWA NCHI YETU!!!! Semboja, Mohamed Jumanne Sent: Saturday, August 04, 2012 3:32 AM To: Tanzanet Subject: [tanzanet] Mwalimu afukuzwa kazi kwa kuzungumza Kiswahili Arusha Ninaomba WIZARA YA ELIMU iwe makini na wawekezaji katika secta ya elimu, hasa kwenye shule ambazo zinatoa msaada kwa watoto wakitanzania ambao familia zao hazina uwezo wa kifedha, kwa mfano ninaomba mmiliki wa shule ya St Jude apate muda wa kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake wakitanzania kwani kimsingi wamekuwa wakiteswa, kukandamizwa na kupuuzwa wanapodai haki na maslahi bora kazini kwao. Shule hii utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha kuendesha shule, kwa wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa mara na kulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila shule kuweka wazi kwa mfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi, wafadhili huchangia kiasi gani cha fedha, kukatazwa kuwasiliana na mfadhili, kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu pato na matumizi ya uzalishwaji wa fedha kupitia wewe na familia yako? Hata hivyo picha za familia zinazalisha fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihali familia haifaidiki kwa uuzaji huo wa sura zao ughaibuni? Kinachosikitisha zidi ni pale mfanyakazi anapoachishwa ,shule inaendelea kitumia picha za wafanya kazi na familia zao kuzalisha fedha nyingi za kigeni bila ridhaa wala fedha hizo kuwafaidisha wenye picha, na kutojali kuwa kitendo hicho kinyume na sheria. Pia picha hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wa muafrika, kwani sura za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedha zisizojulikana ni kiasi gani na kwa faida ya nani? tena ulazimisha vitendo visivyo halisi na maisha yetu mfano unalazimishwa kucheka ukichukuliwa picha ilihali mapato uzalishayo hujui na ukikataa kutekeleza unatishiwa kufukuzwa kazi, wanafunzi ushikishwa zawadi zisikuwa zao na kupigwa picha na uzalisha kiasi cha fedha bila ridhaa wafunzi wanapohoji hupewa adhabu au kutishiwa kufukuzwa. Kama hiyo aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchi bila sababu za msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni kinyume na sheria za nchi mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa familia moja tena kwenye nafasi za juu na kutoweka wazi taaluma zao wakiwaaminisha kuwa ukiwa mzungu basi we msomi wa kila kitu, kinyume na sheria ya ajira nchini, pia shule imekuwa mara kadhaa haieshimu sikukuu za kitaifa bila sababu za lazima na kutojali wala kuthamini mchango wa waasisi na wazalendo waliopoteza maisha kujenga utaifa, amani na umoja wa Tanzania, cha kushangaza shule ujiamulia siku za mapumziko ya wafanyakazi na wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza hivi shida inaweza tulazimisha kufuata sheria za wawekezaji na kupuuza sheria za nchi yetu Tanzania? Linalosikitisha zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumizi ya lugha ya kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibu kwa kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hata kufika mbali zaidi na kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa kosa ni kuzungumza kishwahili na wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria za nchi usiovumilika. Hata hivyo nataka wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimili mkubwa wa kujenga umoja na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata mafanikio, kama awa amini wakajaribu kuwekeza Somalia na kuwasaidie watoto wa Somalia wenye shida kubwa ya elimu, ilo linge ondoa jeuri yao ya kupuuza sheria za Tanzania. Kitendo cha shule hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu wao wa fukuza fukuza waliyonayo hasa kwa watanzania. Shule hii huwatumia viongozi wazalendo kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule kuendelea na dharau na kupuuza sheria za nchi zenye maslahi kwa wazalendo, wale wote watakaonyesha uzalendo kama mimi wakuonyesha kukerwa na kuchukua hatua ya kuhoji na kutetea sheria za nchi na watanzania dhidi ya upuuzwaji wa uzalendo, haki, utu, lugha ya taifa, maslahi ya kiwango cha utumikishwaji, niliishia kufukuzwa kwa kosa la kuongea kishahili na wanafunzi. Ushauri wangu kwa wizara ya elimu. Kwanza kupandisha mshahara na mazingira ya kazi serikalini ilikuvutia waalimu wote toka shule binafsi kwani wangi wamechoshwa ni manyanyaso ya waajiri. Pili kufanya ukagua si wa taaluma tu bali pia mfumo wa uajiri na maslahi ya watanzania waajiriwa kwenye shule zinazomilikiwa binafsi kwa misaada ya watu toka ughaibuni. Tatu iwe na utaratibu wa ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya shule zinazopata fedha toka kwa wafadhili kwani shida za watanzania zimekuwa zikinufaisha wachache na kutengeneza ajira ya watu wasiona sifa za kufanya kazi ughaibuni na kuja kufanya kazi ambazo wazalendo wanaweza kuzifanya. Nne kusisitiza hasa shule binafsi nchini kuthamini lugha ya kishwahili, kuheshimu sheria za ajira, kuheshimu sikukuu za kitaifa na kuheshimu, kulinda tamaduni na vipaji vya watanzania kwa manufaa ya Tanzania. Ni kweli tarere 15/06/2012 nimefukuzwa kazi ya kufundisha (ualimu) St-Jude-Arusha kwa kosa la kuzungumza Kiswahili. Uzalendo gharama nimeamua kujitoa kwa kutetea nchi yangu Tanzania. Mwalimu Daniel Urioh. Kwa undani zaidi piga :+255 755 379 737 Chanzo: http://www.kajunason.blogspot.no/2012/08/mwalimu-afukuzwa-kazi-kwa-kuongea.html

Saturday, August 4, 2012

WABUNGE MAFISADI WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WATAJWA

WABUNGE MAFISADI WATAJWA mwananchi.co.tz | Jul 29th 2012 8:14 AM SPIKA AVUNJA KAMATI YA NISHATI, WAZIRI AELEZA WALIVYOITAFUNA TANESCO Kizitto Noya na Boniface Meena, Dodoma WAKATI wabunge wakitoa tuhuma nzito dhidi ya wenzao wanaodaiwa kujihusisha na ufisadi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), imebainishwa kuwa wabunge wenye tabia hiyo ni watano, watatu kutoka chama tawala CCM na wawili upinzani. Habari zilizopatikana jana mjini Dodoma zimeeleza kuwa baadhi ya wabunge hao wanatoka katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, huku wengine wakitoka Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma. Kwa mujibu wa taarifa hizo, wabunge hao wamedaiwa kuwa wamekuwa wakitumia nafasi zao za ubunge na ujumbe wa kamati kufanya biashara na Tanesco na kutetea mafisadi ndani ya shirika hilo la umma. Gazeti hili limefanikiwa kupata majina ya wabunge hao, ambayo leo hatutayataja kwa sababu za kitaaluma. Baadhi ya wabunge waliochangia hoja hiyo bungeni juzi na jana walisema kuwa, wanawafahamu wabunge hao kwa majina, lakini hawapendi kuwataja kwa kuwa siyo wakati mwafaka. Moto wa kutaka kutajwa kwa majina ya wabunge hao ulikolezwa jana na Mbunge Vita Kawawa wa Namtumbo(CCM) aliyeomba Mwongozo wa Spika, akitaka jambo hili lijadiliwe na Bunge na kupendekeza kuwa, Kamati za Bunge zinazotuhumiwa kwa rushwa zivunjwe. “Waheshimiwa wabunge wamejadili suala hili kwenye wizara, lakini kwa mujibu wa kifungu cha 55 (3)f mbunge au waziri anaweza kutoa hoja ili jambo fulani lijadiliwe. Sasa naomba kutoa hoja ya kujadili suala hilo," Kawawa alisema. Aliliomba pia Bunge likubali kuivunja na kuiunda upya Kamati ya Nishati na Madini na kamati nyingine zilizolalamikiwa kwa rushwa. Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge. Baada ya hoja hiyo kuungwa mkono Spika wa Bunge, Anne Makinda alisimama na kukubali hoja hiyo ya Kawawa na kutangaza kuivunja Kamati ya Nishati na Madini. Spika Makinda alisema ameiagiza Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge kutengeneza kanuni za kuwadhibiti wabunge wenye tabia hiyo ya kupokea rushwa kutoka kwa watu mbalimbali ili kutimiza matakwa yao binafsi. "Ninakubali kuivunja Kamati ya Nishati na Madini na zingine ambazo zitatajwa kwenye tuhuma hizo. Nalipeleka pia suala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, halafu kama ni kutajwa (wabunge hao), basi tutapata mwongozo wa kamati hiyo." alisema Spika Makinda na kuongeza: "Nasema kwa dhati kabisa, kitendo hiki hakikubaliki ndani ya Bunge hili. Wabunge mkae vizuri. Kama kuna baadhi yetu wanaenda huku na huku kujitafutia masilahi binafsi, tutawezaje kuisimamia Serikali?" Mbunge Zedi Baada ya Spika kutangaza kuvunja Kamati ya Nishati na Madini, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Seleman Zedi alisema kuwa ameshtushwa na uamuzi huo na anasubiri uamuzi wa Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge. "Nimeshtushwa sana na uamuzi huo, lakini tusubiri Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge," alisema Zedi. Waziri Muhongo Akihitimisha hoja ya wizara yake bungeni jana, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa baadhi ya wabunge ambao wanashiriki kwenye vikao vya uamuzi vya Tanesco kama wajumbe, wamekuwa wakilihujumu shirika hilo kwa njia mbalimbali ikiwamo kufanya nalo biashara. "Shirika liliwahi kulipa Pauni za Uingereza 50,000 kwa ajili ya kununua vipuri, lakini kilicholetwa nchini ni masanduku ya misumari,” alisema Profesa Muhongo na kuongeza; “Hata katika nguzo za umeme kuna biashara inaendelea. Tunajua kuwa nguzo hizo zinazalishwa Iringa na kupelekwa Mombasa kisha kurudishwa nchini kwa maelezo kwamba zimetoka Afrika Kusini." Waziri Muhongo alisema kuwa mbali na ufisadi huo, baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini wamewahi kuliuzia shirika hilo matairi ya magari kwa bei kubwa, bidhaa ambayo hata hivyo alisema haina ubora unaokubalika. "Baadhi ya wabunge wanafanya biashara na Tanesco; niseme tu kuwa, hii siyo sahihi. Lakini niombe kwamba mjadala huu tuufunge kwa sababu, tayari tumekabidhi suala hilo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)" alisema Waziri Muhongo. Waziri Muhongo pia alizungumzia jinsi baadhi ya watu na kampuni zinavyoiibia Tanesco kupitia mita za Luku ambapo aliwataja watu hao kuwa ni pamoja na Shule za St. Mary's zinazodaiwa Sh10.5 milioni, Access Bank, Tawi la Tabata Matumbi Sh13.8 milioni na Hoteli ya Akudo Paradaise ya Kariakoo inayodaiwa Sh25.5 milioni. Alisema kuwa baada ya kubainika kwa wadaiwa hao hutumia umeme kinyume na utaratibu,wahusika wote walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi baada ya kufanyika kwa uchunguzi. “Baada ya kufanya uchunguzi na kubaini kuwapo kwa watu wanaotumia umeme bila kulipia na kuisababishia Tanesco hasara, tumeamua kuwachukulia hatua ikiwamo kuwafikisha polisi,” alisema Profesa Muhongo na kuongeza: “Inaonyesha wazi kwamba wizi wa umeme wa Luku umekuwa ukifanyika mara kwa mara na kwamba baada ya kuwakamata hawa, uchunguzi utaendelea na wengine watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.” Jenista Mhagama Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama alisema kuwa, amepokea kwa masikitiko taarifa hizo za wabunge wa CCM kuingia katika tuhuma hizo, lakini akasema namna nzuri ya kushughulikia tatizo hilo ni vyombo vya dola kufanya uchunguzi makini ili kujiridhisha na kisha hatua za kisheria kufuatwa. "Ni taarifa mbaya kwa kweli, lakini mimi niiombe Serikali itusaidie kufanya uchunguzi ili ukweli ubainike na hatua zichukuliwe," alisema Mhagama. Mbunge Silinde Naye Katibu wa Wabunge wa Chadema, David Silinde alisema: "Kwa kuwa tumesikia, kama kambi tutafanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo. Tutakaa kikao cha kuamua nini cha kufanya. Pia tutatoa tamko juu ya mwenendo mzima wa hizi tuhuma na Bunge kwa ujumla.” Zitto Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma ambayo imeunganishwa kwenye tuhuma hizo, Zitto Kabwe, alisema tuhuma hizo anazisikia, lakini anaziona kama siasa za majitaka kwa sababu zinarushwa bila ushahidi wowote. "Hakuna hata mbunge mmoja aliyesimama kusema nani amehongwa nini. Mimi binafsi sijahongwa na mtu yeyote wala mimi sijamtetea mtu isipokuwa natetea taratibu kufuatwa," alisema. Zitto alibainisha kuwa anaamini tuhuma hizo zimetokana na hasira za yeye kupinga posho za wabunge na sasa wameona hilo ndilo eneo la kumkomoa. "Kwa kuwa ‘my conscious is clear’, (dhamira yangu safi) sina mashaka, uzushi, uongo na siasa za majitaka hizi zitaumbuliwa na ukweli. Hata hivyo, kwa kuwa tuhuma hizo zinasemwa juu juu tu, tutataka vyombo vya dola vichunguze na ikithibitika hatua zichukuliwe," alisema na kuongeza: "Kwangu mimi naona hizi ni siasa za urais na hasira za posho. Wenye kutaka urais wa vyama vyote na wapambe wao, wameungana kunichafulia heshima yangu. Wabunge wenye njaa ya posho, wameungana kunikomoa. Ukweli una tabia ya kutopenda kupuuzwa. Mwalimu Nyerere (Julius) alisema katika andiko lake la 'Tujisahihishe'.” Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini(Chadema) alishauri pia Spika wa Bunge kutumia Kamati ya Maadili kuchunguza tuhuma hizo kwa kuwa hazipaswi kuachwa zikapita hivihivi. John Cheyo Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali, John Cheyo alisema anasikitika kuona Bunge ambalo kimsingi ni kitovu cha uadilifu limeanza kuvamiwa na mafisadi. "Very unfortunate, (bahati mbaya sana) Bunge ambalo ni kilele cha uadilifu, nyumba ya waheshimiwa, ambako kunatarajiwa high level of intergrity (uadilifu wa hali ya juu), kuanza kutumika kama perpets (vibaraka) wa mafisadi," alisema. Cheyo aliongeza: "Ninalaani sana kitendo hicho, lakini niwaambie viongozi wapya wa Wizara ya Nishati na Madini kuwa, waendelee kufanya kazi kwa uadilifu na nguvu yao ni wabunge wengi wema, ambao watawaunga mkono. Wasikate tama," alisema. Mjadala ya wabunge Mbunge wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda aliliomba Bunge kufanya uchunguzi ili kuwabaini wabunge wanaojihusisha na vitendo vya rushwa. Alisema baadhi ya wabunge wanatumia nafasi zao vibaya kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ili kuiyumbisha Serikali. “Namwomba Spika na timu yake yote ikaona kuna haja ya kufanya uchunguzi kwa wabunge ili kuweza kuwabaini wanaotumia nafasi zao vibaya kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ilikuiyumbisha Serikali ,” alisema Shibuda Mbuge Kangi Naye Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora alitaka Waziri wa Nishati na Madini awataje wabunge aliowatuhumu ili kuonyesha usawa hasa baada ya kuwataja kwa majina watuhumiwa wengine katika ufisadi wa Tanesco na wale wanaoliibia umeme shirika hilo la umma. "Tunaomba waziri asema kwa nini asiwataje hao wengine wakati tayari ametutajia kina Freddy na Veronica William Mhando na taasisi za St Mary? " alihoji. Hoja hiyo ya Lugora ilitupwa na Spika wa Bunge Anne Makinda aliyesema kuwa jambo hilo lina taratibu zake. Kamata Vicky Kimata (Viti Maalumu) nusura amwage machozi bungeni juzi jioni, alipozungumza kwa uchungu kupinga hatua ya wabunge hao kujihusisha na ufisadi, huku akieleza kuwa nchi imefika pabaya. 'Watanzania tumefikia hapo! Watu wanatengeneza mgawo wa umeme ili kujipatia hela, Jamani...jamani.. Hammwogopi hata Mungu!" Said Mussa Zuberi alipendekeza itungwe sheria ya kuwanyonga mafisadi na wahujumu uchumi kwa kuwa matendo hayo pia ni uuaji. "Katika taifa letu tuna wadudu sijui tuwaite mchwa ambao wanaharibu yaliyotengenezwa kwa maslahi yao. Nawashauri wananchi kwa kuwa sasa tuko kwenye suala la Katiba, wasisahau kupitisha sheria ili watu wahujumu uchumi tuwaue, tena kwa risasi.