Wednesday, March 4, 2009

REGINA CHILUBA KAULA WA CHUYA KWA UVIVU WA KUCHAGUA !



Page last updated at 17:52 GMT, Tuesday, 3 March 2009

Zambian ex-leader's wife jailed

Frederick Chiluba is also on trial for corruption. The wife of Zambia's former President Frederick Chiluba has been jailed for three-and-a-half years.
Regina Chiluba was found guilty of receiving stolen state funds to buy three houses and a commercial property while her husband was in office. She married Mr Chiluba after he stood down in 2001, having served two terms. The BBC's Musonda Chibamba in Lusaka says Mr Chiluba, who is also on trial for corruption, shook his head as the magistrate read out his verdict.

Our correspondent says Mrs Chiluba - usually a glamorous dresser - was wearing a simple traditional "Chitenge" outfit in court in the capital, Lusaka. These were serious allegations and were casually explained by the accused Magistrate Charles Kafunda.
She continuously mopped her face with a handkerchief during the two-hour judgement.
Every available seat in the court was taken up and many more people stood at the back of the room while others blocked the door, our reporter says.
A shocked silence filled the court when the conviction was read out.
"These were serious allegations and were casually explained by the accused, and I now convict you accordingly and sentence you to three-and-half years simple imprisonment," AFP news agency quotes Magistrate Charles Kafunda as saying.
Some relatives began to silently weep and had to be helped out; others began to sing Christian songs, our correspondent says. Soon after judgement was passed, a court clerk took Mrs Chiluba's fingerprints while the former president joined her in the dock.
She was then led to a waiting car and driven to the Lusaka Central Prison to begin her sentence.
The court ordered that all the properties in question be forfeited to the state.
Her lawyer has indicated that he will appeal against the sentence in Lusaka's High Court.
Mrs Chiluba was also convicted of receiving a television set that the prosecution proved belonged to the state and for failing to explain how she came to have nearly $100,000 in her personal bank account.
Her husband, whose immunity from prosecution was lifted in 2003, denies stealing millions of dollars of state funds. Levy Mwanawasa, who launched a high-profile campaign after succeeding Mr Chiluba in 2001, died last year. President Rupiah Banda has promised to follow in the footsteps of his predecessor.

Tuesday, March 3, 2009

MAHAKAMA KUU YA RUFANI YA SHIRIKISHO NCHINI MAREKANI

Tarehe 25 Februari, 2009 tulitembelea Mahakama Kuu ya Rufaa ya Shirikisho la Marekani (Federal Supreme Court) ambayo ndio mahakama ya juu kabisa ya rufaa nchini humu, iliyopo kati ya First Street na Second Street, Washington DC., U.S.A. Mji huu, ambao serikali yake ya Mtaa huuita Washington Metropolitan Authority (hauitwi city wala manispaa) una wakazi wanaokisiwa kuwa 600,000 kwa mahesabu ya mwaka 2008.

Jambo la kwanza kuliweka wazi katika mhimili huu wa Dola ni kuwa Majaji wa Mahakama Kuu nchini humu hawana umri wa kustaafu. Hivyo Jaji anapoteuliwa kufanya kazi hiyo ni ya umri wake wote uliobaki hadi ashindwe mwenyewe, mathalan kiafya.

Kwa upande wa Mawakili wa Mahakama hii ya juu kabisa nchini Marekani, sifa yao ni kuwa ni lazima wawe wametumikia wadhifa huo wa uwakili (baada ya kupasi Mitihani ya American Bar Association) kwa miaka mitano. Baada ya hapo wanaomba kwa Mahakama hiyo kuwa Mawakili wa Mahakama hii. Wanapokubaliwa ndio wanatambulishwa rasmi kuwa ni Mawakili wa Makama ya Rufani ya Shirikisho. Siku tulipokuwepo, walitambulishwa Mawakili zaidi ya 10 wa Mahakama hiyo. Hiyo maana yake ni kwamba, kuanzia utambulisho wao huo, sasa wanaweza kuwakilisha wateja katika Mahakama hiyo. Wamekuwa Maofisa wa Mahakama ya Rufani ya Shirikisho.

Katika nchi hii ya Marekani, Katiba yao inaruhusu sana Utaratibu wa Mizani ya Dola (checks and balances) ndio maana majaji wao majimboni wanachaguliwa na wananchi kwa kura, na kisha kumuachia Gavana wa Jimbo kuteua, na Bunge lake kuidhinisha. Na vivyo hivyo Majaji wa Mahakama ya Shirikisho huteuliwa na Rais wa Marekani na kuidhinishwa na Bunge (senate). Kwa maana hiyo, Rais anakuwa si mwenye kauli ya mwisho juu ya uteuzi wa Majaji nchini humu, tofauti sana na nchi kwetu Tanzania ambako Rais huteua Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa; japo hana uwezo wa kuwaondoa kikatiba, anao uwezo wa kuwahamisha atakavyo. Na kuhamishwa kwa Jaji hakuna tofauti na kuondolewa kwa sababu kwa kipindi chote atakachokuwa amehamishwa, hataweza kufanya kazi zake kama Jaji wa Mahakama.

Tulipata fursa ya kusikiliza kesi iliyotoka Hawaii iliyohusu masuala ya Ardhi. Katika Nakala ya Kesi hii kutoka mahakama za chini, kumetolewa maelezo kwa mfano kwamba mwaka 1898 Wamarekani walipoivamia nchi ya Hawaii ilikuwa na watu zaidi ya laki nne (400,000) ambao hadi kufikia miaka thelathini baadaye, walibaki 78,000 tu kutokana na ukandamizaji waliopitia wa Wamarekani.

Mambo niliyoweza kuyashuhudia katika Mahakama hiyo ya juu kabisa nchini Marekani ni kama yafuatayo:

1. Mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za kutoka majimboni, ambazo zimeamuliwa kwa kutumia sheria za majimboni huko tu. Mahakama za rufaa za mwisho kusikiliza kesi hizi ni Mahakama za Rufaa za Majimbo husika (State Supreme Courts).

2. Kuna Waheshimiwa Majaji tisa wa Mahakama hii wanaokaa kwa wakati mmoja. Katika idadi iliyokaa siku hiyo, kulikuwa na Mwanamama mmoja Mheshimiwa Jaji Ruth Bader Ginsburg. Mama huyu alituacha hoi kwa kuongoza kuuliza maswali kwa sababu ni majuma matatu tu nyuma yake alitoka kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe hatari (malignant tumour) tumboni mwake.

3. Waingiapo Majaji hawa Mahakamani, wanatumia utamaduni wa Kiingereza wa Karani kuita "Court Rise!!!!!" Lakini yeye alitumia maneno yanayofanana na hivyo wote tuliokuwamo tukasimama kwa heshima yao.

4. Lakini wakati wa kumaliza kusikiliza kesi hiyo, waheshimiwa majaji hawakutoka nje. Walibaki vitini, ila sisi wasikilizaji na waandishi wa habari ndio tuliotoka tukiwaacha Waheshimiwa ndani.

5. Pia Washeshimiwa Majaji wana uhuru wa kumtupia maswali msemaji wa wakati huo; awe mshitaki au mshitakiwa (au mawakili wao). Jambo hili nimeona geni sana kwani Tanzania Majaji husikiliza tu hoja zitolewazo toka pande mbili.

6. Chumba cha Mahakama hii ya juu kabisa nchini Marekani sio kikubwa kama nilivyofikiria. Ni kama chumba cha kuweza kuketi watu 300 hivi kwa makisio. Nilitaraji kuwa Mahakama hii ingekuwa na chumba kikubwa zaidi ya hiki.

7. Kuna ulinzi mkali sana katika jengo hili kuanzia nje hadi ndani. Kwa wasikilizaji wa kesi, kila itokeapo kesi hutakiwa kusimama foleni nje kadri watu wafikavyo. Ifikapo saa 3.00 asubuhi ndio askari huruhusu watu kuingia katika chumba cha kuchunguza usalama na kisha chumba cha kuchunguzwa usalama tena kabla ya kuruhusiwa ukumbini.

8. Hairuhusiwi kuvaa makoti wala kofia Mahakamani. Vyote hivi huhifadhiwa katika chumba maalum kabla ya kuingia. Chumba cha hifadhi kila vikabati ambavyo msikilizaji anatakiwa kulipia $0.25 (senti ishirini na tano ambazo kwa Tanzania ni kama Tshs.250/=) ili upate kuvihifadhi vifaa vyako kwa usalama zaidi. Na kila ukitaka kufungua kikabati hicho (Locker), inakubidi ulipie $0.25 nyingine. Mimi yalinikuta kwa sababu nilisahau kuvua kofia baada ya kufunga kikabati. Nikatakiwa kurudi kuhifadhi kofia. Ndipo nikakuta nalazimika kutoa senti ishirini na tano nyingine ili nifungue tena. Nikasema kwa hili tu basi Mahakama Kuu hii inajipatia mamilioni kwa mwaka. Mahakama hii kwa nchi hii huwa inakaa kwa siku tatu kwa kila wiki na kila mwezi isipokuwa wanakuwa na likizo muda fulani tu. Kwa hiyo huduma ya Mahakama hii ni kama ofisi nyingine. Tofauti kwa mfano na Tanzania ambako nadhani Mahakama ya Rufani haikai kwa ratiba ya kila wiki kama hii.

Kiongozi wetu katika msafara huu alituarifu kuwa Mahakama hii ni katika majengo mapya eneo lile (kati ya majengo ya mihimili mikuu ya dola). Amesema jengo la Mahakama lilikamilika ujenzi mwaka 1935. Jirani na Jengo hili kuna Maktaba Kuu ya Wabunge wa Marekani (Library of Congress, ambayo ina majengo makubwa matatu; Madison Bldg., Jefferson Bldg., na Adams Bldg.) na linatazamana na Bunge la Marekani (Capitol Hill). Majengo yote haya yapo katika Mji Mkuu wa Serikali ya Marekani, yaani Washington District of Columbia (DC). Mji mkuu wa biashara katika nchi hii ni New York City, ulio kaskazini ya huu.

Monday, March 2, 2009

MAKALA YA AFYA BORA NA. 8

Article No. 8 kutoka kwa Dr. Wilbert Bunini Manyilizu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Tanzania.

Tarehe 2 Machi, 2009.

Mwendelezo wa article No 7

Mfululizo wa matukio tangu kuchoma plastiki hadi afya kuharibika

Sumu ya dayoksini hutengenezwa tu pale plastiki inapochomwa. Plastiki inapokuwa inaungua ndipo sumu hiyo hutokea kama mvuke au moshi. Moshi huu huingia kwenye pua ya yeyote aliyepo karibu hata yule wa mbali atakayefikiwa. Huvutwa na kuingia mapafuni ambapo huziingia chembe chembe mbalimbali zenye asili ya kuwa na mafuta (adipose tissues). Hunata kwenye chembe chembe hizo, na hatimaye kuingia ndani ya chembe chembe katikati kabisa kwenye kiini cha chembe chembe (nucleus). Hapa hujichanganya na kujifanya sehemu asilia ya chembe chembe hizo. Chembe chembe asilia za binadamu zina kazi za kuendesha mambo yote ya kifiziolojia (kiutendaji), chembe hizi zinapokuwa zimevamiwa na sumu hii huanza kubadilishwa tabia na utendaji wake wa kazi na kuanza kufanya kazi zingine ambazo zinakuwa zimetumwa na huyu mgeni aliyejichanganya, na huanza kuzalisha magonjwa ambayo yametajwa kidogo hapo awali (article 7) na mengine katika aya zifuatazo.

Moshi wa sumu ambao haukuingia kwenye pua za watu hupeperushwa kwenye hewa mpaka umbali wa kilomita mamia kama vipeperushi vidogo sana. Sumu hii inakofikia hunata kwenye majani ya mimea na mazao mbalimbali. Ng’ombe, mbuzi, nguruwe na wanyama wengine wanapochunga hutumia sumu hii, nayo huwaingia na kutuama kwenye chembe chembe zenye asili ya kuwa na mafuta katika miili ya wanyama hawa. Sumu nyingine inayopeperuka huishia kwenye miti, maziwa (lakes) na bahari na vyanzo mbalimbali vya maji. Huko nako kuna wanyama kama samaki na wadudu wengine, hawa nao hupata dozi ya sumu na kukaa nayo katika chembe chembe za mafuta. Siku nyingine mtumiaji wa samaki, nyama, maziwa yenye mafuta (creamy) hupata sumu hii kupitia mzunguko huu. Hapa madhara ya sumu hii huja kwa binadamu. Hii ni kwa sababu sumu hii haiharibiwi na aina mbalimbali za mazingira nje na ndani ya wanyama na binadamu.

Sumu hii inapokuwa sehemu ya kiini cha chembe chembe huanza kuharibu mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Kwa sababu chembe chembe nyeupe (maaskari wa mwili dhidi ya magonjwa) za ulinzi hulewa sumu na dawa inayotengenezwa kushindana na maadui wageni pia hupungua. Mfumo wa uzazi wa kawaida huharibiwa, hamu ya kufanya mapenzi hupotea (loss of libido). Sumu hii hupunguza uwezo wa uzazi na kupoteza uwezo wa kuchukua mimba mpaka miezi tisa, nyingi hutoka kabla ya hapo. Watoto wa kiume wanaobahatika kuzaliwa huwa na homoni za kiume kidogo kuliko kawaida, na baadaye huwa na uwezo mdogo (kutokana na kuwa na kiwango kidogo cha homoni ya testosterone) wa kuzalisha mbegu za kiume za uzazi. Watoto huwa hawana uwezo pia wa kutosha katika masomo (learning disabilities) kwa sababu ya sumu hii. Makuzi ya watoto kama ndiyo waathirika huvurugwa, kwani tezi ya makuzi (thyroid gland iliyoko mbele kwenye shingo) huathirika kwa sumu, neva za fahamu huharibiwa. Sumu hii huleta kansa katika dozi ndogo sana inayoweza kudhaniwa haiwezi kuleta madhara. Sumu hii huwa na tabia ya kuhamasisha uanzishaji wa chembe kichaa za kansa (potent cancer promoter) kwa sababu huzibadili tabia homoni zinazohusika na kukua.

Kukua kwa mtu maana yake ni kugawanyika na kuongezeka kwa idadi ya chembe chembe na kukua kulingana na zile za awali. Sumu huzifanya chembe chembe hizi ziwe nyingi isivyo kawaida badala ya kugawanyika na kuzikuza kwa kawaida mtu aonekane kaongezeka (yaani kakua), zenyewe huzifanya zigawanyike zikiwa chembe mbovu zenye kichaa (zenye tabia isiyorekebishika) zinazozaa haraka kuliko kawaida; hizi ndizo zinazoitwa chembe chembe za kansa. Hivi ndivyo sumu ya dayoksini inavyoweza kusababisha aina mbalimbali za kansa katika kiungo chochote ambacho huwa kina tabia ya kukua.

Habari za utafiti katika wanyama

Utafiti uliofanywa kwa wanyama wa porini waliopewa sumu hii kwa kiwango kidogo sana unaonesha kuwa walipata kansa za viungo mbalimbali zikiwemo kansa ya ini, tezi za adrena, thairoidi, kansa ya ngozi, mapafu, pua na kinywa. Kinga dhidi ya magonjwa iliharibika kwa maisha yote, pale ilipojaribiwa kwa wanyama wenye mimba kwa kutoa sumu hii dozi moja kwa kiasi kidogo mimba ziliharibika. Kuondoa tatizo hili katika jamii za kimaskini, inahitaji nguvu ya kutosha na ushirikiano katika nyanja mbalimbali, kuanzia mtu binafsi, jamii, sekta kama za afya, mazingira na wanasiasa. Tatizo likionekana ni tatizo kwa wote ndipo nguvu inaweza kuelekezwa huko. Kama msomaji anaweza kuona hili naamini hawezi kukaa kimya, na huu ndio mwanzo wa mapambano dhidi ya adui maradhi. Mwanafunzi mzuri hahitaji kusubiri mwalimu aje amwanzishie uelewa na utekelezaji bali mwalimu humsaidia kurahisisha kuelewa. Msomaji anaweza kufanya kitu hapo alipo, ili mradi tu aepuke kuahirisha. Inawezekana.

WADAIWA SUGU NI WENYE UWEZO WA KULIPA BILI!

AIBU ILIYOJE kwa wenye uwezo wa kulipa bili kukatiwa maji?


Evance Ng’ingo

Daily News; Sunday,March 01, 2009 @19:00
Maeneo ya Dar es Salaam ambayo yanakaliwa na watu wenye kipato cha kutosha yameelezwa kuwa ndio maeneo yenye wadaiwa sugu wa ankara za maji za Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO).

Akizungumza na waandishi habari jana katika ofisi za Dawasco, Meneja Biashara wa Kampuni hiyo Raymond Mdoe alitaja maeneo hayo yenye wadaiwa sugu kuwa ni pamoja na Mbezi Beach, Masaki na Kijitonyama.

Mengine ni Makongo Juu, Tegeta, Mwananyamala na Sinza. Amesema maeneo hayo takribani asilimia 50 ya wakazi wake hawalipi ankara za maji. Mdoe amesema kampuni yake inatoa siku saba kwa wadaiwa hao sugu kulipa madeni yao au la huduma hiyo itakatwa

WOMEN LEGAL AID CENTRE (WLAC) MIAKA 20

HEKOOOOOO na HONGERA SANA WILAC!

Ikunda Erick

Daily News; Sunday,March 01, 2009 @19:00
Wafanyakazi wa WLAC, wakitumbuiza kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto.jpg


Utawala wa sheria ni nguzo muhimu inayoongoza Tanzania katika kuhakikisha haki za binadamu zinafuatwa bila ubaguzi wala upendeleo wa makundi yaliyopo ndani ya jamii. Makundi hayo ni kama vile jinsia, kabila, tabaka, rangi, dini na kwamba haki kama vile kuishi, kumiliki mali, ardhi, kuwa huru, kulindwa, elimu, kuolewa/kuoa, kutopata mateso, ukatili na kudhalilishwa ni vitu vya msingi kwa binadamu.

Lakini pamoja na sheria na Katiba ya nchi kuyataja hayo na kusisitiza, bado kuna baadhi ya wanajamii ambao huzivunja na kukandamiza baadhi ya makundi katika jamii, kwa manufaa binafsi. Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), ni shirika binafsi la kujitolea lililoanzishwa na kusajiliwa rasmi mwaka 1994, kwa lengo la kusaidia makundi hayo katika jamii kupata msaada wa kisheria ili kuondoa unyanyasaji uliokithiri.

Uanzishwaji wa kituo hicho ni mwendelezo wa kitengo cha msaada wa sheria katika Shirika la Uchumi la Wanawake (Suwata) lililoanzishwa mwaka 1989, likiwa na njozi ya kuona jamii inaheshimu haki za wanawake na watoto. Wiki iliyopita Dar es Salaam, WLAC walifanya maadhimisho ya miaka 20 ya kituo hicho ambacho kimekuwa Nyota ya msaada wa kisheria katika kufanikisha urejeshwaji wa haki za makundi hayo zilizoporwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, Scholastica Jullu ambaye kitaaluma ni mwanasheria, anasema tangu kuanzishwa kwake, wanawake 39,670 wamefanikiwa kupewa msaada wa kisheria ambapo 39,470 kati ya hao wamepata haki zao mahakamani.

Katika hao waliopata haki mahakamani ni pamoja na wale wajane waliofiwa na waume ambapo mara baada ya msiba, ndugu wa mume waliwanyang’ang’a mali na kuwaacha wakiwa na masikini. Scholastica anasema ingawa sio wote waliofika moja kwa moja katika ofisi za shirika hilo ambazo ziko kwenye maeneo tofauti nchini, lakini wapo walioweza kupewa msaada wa kisheria kwa njia ya simu.

“Tunashukuru tumeweza kuona manufaa ya kituo hiki, tumewakomboa waliokata tamaa ya maisha kwa kutojua ni wapi pa kwenda kuomba msaada wa sheria, wengine waliogopa gharama za kuendesha kesi, lakini sisi tunasaidia bure”, anasema Scholastica.

Anasema WLAC imekuwa msaada mkubwa ndani ya jamii kwa kuwa kwa hao waliokwishapata msaada wa kisheria, nao wamekuwa wakiwaambia na wengine wanaonyanyaswa juu ya kituo hicho, hivyo kuwawezesha nao kupata haki zao zilizopotea. Kwa kushirikiana na mashirika mengine ikiwemo serikali, wamefanikishwa kupitisha sheria zinazomlinda mwanamke, hadhi, haki na utu wake.

Mwaka 1998 sheria ya makosa ya kujamiiana ilirekebisha sheria tano zinazohusu mwenendo na namna ya kushughulikia makosa ya kujamiiana au makosa yanayoweza kutendeka, na hivi sasa marekebisho hayo yameingizwa katika sheria husika.

Pia ni kupitia WLAC, wameweza kufungua kesi ya mfano mahakamani ya kutaka ufafanuzi juu ya hali ya utata wa kikatiba uliopo katika sheria ya mirathi ya kimila. Katika sheria hiyo inawanyima haki wanawake wajane na watoto wa kike kurithi mali zilizoachwa na marehemu waume/baba zao, hivyo kufanya haki zao kuporwa na ndugu na kuacha familia ikiwa masikini bila msaada.

Katika jamii, unyanyasaji dhidi ya watoto na wanawake umekuwa ukifanywa na ndugu hasa baada ya mzazi wa kiume kufariki ambapo tumaini na ndoto ya maendeleo huyeyuka kutokana na familia nyingi kuvurugwa na kudhulumiwa haki zao.

Akitoa ushuhuda wa manyanyaso na kudhulumiwa, ambapo WLAC iliingilia kati na kumkomboa, Martha Justine (55) mama wa watoto wawili mkazi wa Segerea, Dar es Salaam anasema baada ya kufiwa na mumewe mwaka 1989, mashemeji walimdhulumu nyumba na mali.

Martha anasema mumewe, alipofariki, alimuachia mtoto mdogo wa mwaka mmoja aitwaye Nyangeta ambaye sasa ni msichana mkubwa anayesubiri kuendelea na chuo Septemba mwaka huu, baada ya kushinda kesi yao.

Akisimulia huku machozi ya furaha yakibubujika, baada ya kupewa msaada wa kisheria na kufanikisha kurudisha nyumba aliyonyang’anywa na hao mashemeji, Martha anasema hakutegemea kama haki yake na marehemu mumewe ingerudi.

“Mume wangu alikuwa mfanyakazi Maliasili, alimiliki silaha na tulikuwa na nyumba ya biashara pale Mwenge kwenye vinyago (Dar es Salaam), lakini kifo chake kilinifanya niwe fukara wa kutupa, ila mahakama imerudisha haki yangu”, anasema Martha. Anasimulia, nyumba hiyo ya biashara shemeji zake waliichukua na kuifanya yao, hivyo hakuweza tena kupata fedha za pango ambazo awali walikuwa wakizitumia kulipia nyumba waliyopanga.

Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu kuondoka kwenye nyumba ya kupanga aliyoishi na mumewe na kwenda kupanga chumba kimoja na kuishi yeye na wanawe. Anasema hali ilikuwa ngumu na ikambidi aanze kufanya vibarua kwenye maeneo mbalimbali kama vya kukata majani ya ng’ombe na kuuza, kuuza maji barabarani na pia alikuwa mpishi kwenye shirika la Tanesco.

Martha anasema akiwa Tanesco, Rais Jakaya Kikwete alitembelea shirika hilo na hapo ndipo aliposhindwa kuvumilia machungu yake na kuangua kilio cha kuomba rais amsaidie jambo ambalo lilikuwa mkombozi wake. Baada ya kulia kwa uchungu, anasema rais alimuita Ikulu na kusikilizwa na wahusika ambapo kupitia WLAC, walimuwezesha kufungua kesi ya mwaka 2005, ambapo Oktoba mwaka jana alishinda na kurudishiwa nyumba yake.

“Sikuwa na kitu, si fedha wala nini ila WLAC walinipa mwanasheria ambaye kila mara nilikwenda naye mahakamani na yeye kuniongoza hatimaye nyumba nimerudishiwa, mwanangu sasa atasoma”, anasema Martha kwa uchungu. Anasema baada ya mahakama kutoa amri hiyo, hivi sasa nyumba hiyo ameipangisha na kodi yake inamsaidia kujikimu yeye na familia yake na fedha nyingine zitampeleka chuo mwanaye.

“Kituo hiki kimefanya hayo yote leo nimekuwa tena mtu, si tegemezi tena kwani ninauelewa wa kujua wapi pa kupata haki, na pia jasho la marehemu mume wangu na mimi limerudi”, anasema Martha. Hivi sasa Martha anauza mkaa na kwamba ule muda wa kuhudhuria mahakamani kwa zaidi ya miaka mitatu, umekwisha na anautumia kufanya mambo mengine ya maendeleo ili kujikomboa yeye na familia yake.

Huo ni baadhi tu ya mifano hai ambayo kupitia WLAC, wameweza kusaidia na kuidhihirishia jamii kwamba vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, na elimu duni ya sheria vinaweza kuifanya jamii kuwa masikini na tegemezi. Hiyo ni hali halisi kwa hapa mjini, ambapo vituo vya sheria na wasomi wengi wako karibu ukilinganisha na maeneo ya vijijini, lakini bado ukatili na unyanyasaji unaendelea kufanywa dhidi ya makundi hayo hata kwa maeneo ya miji.

Mwenyekiti wa kituo hicho Nakazaeli Tenga, ambaye pia ni wakili, anaitaja mikoa 19 yenye ofisi za kituo hicho kuwa ni Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Lindi, Mtwara, Manyara, Mwanza, Ruvuma, Shinyanga, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Dodoma, Iringa, Pwani, Mbeya, Tabora, Singida na Kagera. Nakazaeli anasema pamoja na huduma waitoayo kuwa na mafanikio, bado zipo changamto ambazo zinaendelea kuwa kikwazo kwa huduma hiyo kufika maeneo mengi.

Baadhi ya changamoto hizo ni uelewa mdogo wa jamii kuhusu sheria mbalimbali na haki za binadamu, ambapo wenye shida wengi huenda kituoni wakati kesi zimeshapitwa na muda. Pia uwepo wa sheria za kibaguzi dhidi ya wanawake imekuwa ni kikwazo kikubwa cha ufumbuzi au kuchukua muda mrefu kupata suluhu la tatizo.

Hata hivyo anasema pamoja na vikwazo hivyo zikiwamo pia vya kituo kuendeshwa kwa ufadhili wa nje na kutoweza kujitegemea, lakini bado nia yao ya kuisaidia jamii hususan makundi hayo unaendelea na pia elimu inatolewa ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji.

Ni dhahiri kwamba jamii inapaswa kubadilika na kufahamu kwamba mwanamke katika jamii ni nguzo muhimu ya maendeleo, hivyo wana haki ya kumiliki mali na haki nyingine kama sheria na Katiba ya nchi inavyosema. Ni wajibu wa jamii kuzingatia sheria na kufahamu kwamba hakuna aliye juu ya sheria na kwamba awe mtoto, wanaume au mwanamke wote wana haki sawa mbele ya sheria.

SAFARI YA JIJI LA NEW YORK

Siku ya Alhamisi tarehe 26/2/2009 tulisafiri katika kundi letu la Humphrey Fellows 2008/2009 kutoka Washington DC kuelekea New York kutembelea Umoja wa Mataifa pamoja na ofisi nyingine muhimu. Tulifikia hoteli ya Hampton Inn iliyopo 851 51st na 8th Avenue. Hoteli hii ipo karibu sana na sehemu tatu muhimu. Mojawapo ni Central Park, nyingine ni Broadway na Times Square.

Tulifika Umoja wa Mataifa Ijumaa tarehe 27/2009. Katika matembezi yetu ndani ya Jengo hilo la Umoja wa Mataifa lililopo First Avenue, tulionyeshwa zawadi mbalimbali zilitozotolewa na nchi mbalimbali duniani kwa Umoja huo. Tuliona Busati lililosukwa kwa ufundi mkubwa kutoka Iran, na Kitambaa cha sufu aina ya Kente toka Ghana. Pia tuliona zawadi ya Thailand kwa Umoja huo ambayo ni mfano wa mashua ya Mfalme iliyochongwa kwa ufundi mkubwa. Mwongozaji wetu alituambia kuwa Mashua yenyewe ya Mfalme huyo ni mara kumi ile tuliyoiyona na kwamba imechongwa kwa kutumia mti mmoja tu. Yaani hiyo Mashua halisia ya Mfalme. Pia kulikuwa na zawadi ya kutoka kwa Jamii ya Wahindu, na picha zilizochorwa zilizoashiria vita na amani kutoka Panama.

Katika safu ya Picha za Waliokuwa Makatibu wakuu wa Umoja wa Mataifa kabla ya kuanza kwa Katibu Mkuu wa Kwanza (jina sikulihifadhi), kuna kinyago cha sehemu ya kichwa ya Mfalme wa Namibia, nae pia sikuhifadhi jina lake.

Katika ziara yetu hiyo pia tulipewa elimu juu ya Ofisi ya Haki za Binadamu hapo Umoja wa Mataifa. Bw. Craig G. Mokhiber, Naibu Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu, Ofisi ya New York, alituelimisha juu ya kazi za ofisi yake na kutukumbusha kuwa Umoja wa Mataifa umeundwa ili kudumisha Amani, Kuondoa dhuluma (social justice) na Kudumisha Haki za Binadamu. Katika hayo, amesema ofisi yake ndio imefanikiwa zaidi katika majukumu yake wakati jitihada za kutekeleza yaliyobaki yanakwazwa sana na Wenye Kura ya Turufu (Veto) na nchi zenye uwezo zaidi duniani.

Jiji la New York kwa ujumla wake lina watu wengi mno na majengo marefu mno kiasi kwamba kuiona anga ni nadra kwa sababu ya moshi mzito unaotanda juu kuzuia anga lakini jua litokapo hali ya hewa inakuwa nzuri kwa sababu tulifika wakati wa baridi.

Kama kawaida ya miji mingi sana Marekani, mji huu pia umejaa masanamu ya kila aina ya waheshimiwa wao wa zamani na watu maarufu wengine.

Sunday, March 1, 2009

MICHANGO YA KUCHARAZWA BAKORA WALIMU

2009-02-17 13:12:53
Na Hamisi Kibari
Niliposikia kwa mara ya kwanza kwamba Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera ameamrisha askari kuwacharaza bakora waalimu, swali nililiomuuliza mtu aliyenipa habari hiyo kwa mara ya kwanza lilikuwa hili: ``Huyo mkuu wa wilaya ni mzima kweli kiakili?``
Niliuliza swali hilo kabla hata sijataka kujua sababu za uamuzi huo.

Yule mtoa habari wangu alijibu: \"Pengine ni mzima tu isipokuwa amelewa madaraka... Unajua madaraka na fedha wakati mwingine huwafanya watu wafanye mambo ya ajabu.``

Kwangu mimi, mwalimu kuamriwa achapwe viboko huku wanafunzi wake wakiona au kusikia kwa mbali, hata ungesema amefanya kosa gani ambalo si la kuua mtu, siwezi kukuelewa.

Binafsi nilifarijika kwa hatua alizochukua Rais Jakaya Kikwete, kumtimua kazi mkuu huyo wa wilaya, Albert Mnali.

Nimesikia pia kwamba hatua hiyo ya Kikwete imewagawa wananchi mkoani Kagera. Nimesikia wapo hata wale ambao wanataka kuandamana kupinga kufukuzwa kazi kwa mkuu huyo wa wilaya.

Mimi kama mzazi, ninajua inavyouma kwa mtoto wako kutofaulu mitihani wa kuvuka ngazi moja kwenda nyingine, huku sababu kubwa ikiwa ni uzembe wa walimu.

Lakini pamoja na hayo, DC kuamrisha adhabu ya walimu kuchapwa viboko, inashangaza sana. Inafuta mazuri yake yote, kama yapo, aliyofanya na hivyo adhabu ya kutimliwa kazi ni mwafaka.

Kwa adhabu hiyo, waalimu waliowatendewa `unyama` wanapata faraja angalau kidogo na inawafanya wengine wenye tabia inayoweza kuvuka mipaka yao ya kazi kuwa makini zaidi.

Hakuna ubishi kwamba bwana huyu alilewa madaraka kama alivyonijibu yule mtoa habari wangu kwa sababu, licha ya kukiuka katiba, alikiuka hata kanuni za utumishi wa umma.

Kuhusu Katiba, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ikimlalamikia DC huyo ilisema kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na mikataba ya kimataifa inayolinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora ambayo Tanzania imeridhia inakataa kabisa alichokifanya Mnali.

Ikikariri Ibara ya 13 (6) (e) Tume ilisema ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama ama kupewa adhabu zinazomtweza na kumdhalilisha. Tume iliendelea kusema kwamba adhabu ya viboko hutolewa na mahakama peke yake, tena kwa kosa la jinai linaloainishwa kisheria.

Na kama alivyosema Rais katika hatua ya kumfukuza kazi Mnali, kanuni za utumishi wa umma zinasema kwamba kamati za nidhamu za wilaya na mikoa ndizo zenye jukumu la kumuadhibu mtumishi.

Mbali na madai ya kuchelewa kazini, inaelezwa kwamba Mnali alichukua hatua hiyo kwa kukerwa na wilaya yake kuwa nyuma kutokana na shule nyingi kutofanya vizuri katika kushindisha watoto kwenda sekondari.

Kimsingi, hatua ya watoto kufeli inakera, si tu kwa wazazi bali hata kwa viongozi kama Mnali na inahitaji kuchukuliwa hatua. Lakini hebu tujiulize; kweli kuwachapa walimu bakora ni njia sahihi ya kumaliza tatizo la wanafunzi kufeli darasani? Jibu bila shaka ni hapana.

Mnali alitakiwa kuchunguza chanzo cha wanafunzi kufeli, ambacho hakiwezi kuwa uchelewaji wa waalimu peke yake, kisha akatafuta njia za kumaliza tatizo hilo. Hili si jambo la kukurupuka wala kulimaliza kwa kutumia msuli, kufumba na kufumbua, bali ni kukaa chini na kushirikiana na watalaamu mbalimbali wilayani, hususan maofisa elimu, katika kusaka ufumbuzi.

Je, nini tumejifunza katika sakata hili? Bila shaka yako mengi, lakini mimi nimegundua mawili ambayo ningependa kuyatolea angalizo.

La kwanza ni umuhimu wa kuchukua hatua haraka pale kiongozi wa umma anapolewa madaraka na \'kunajisi\' ofisi, kama alivyofanya Rais Jakaya Kikwete katika kumfukuza kazi Mnali.

Pamoja na kwamba mambo mengine yanahitaji uchunguzi kabla ya hatua kuchukuliwa, lakini siku zote yapo ambayo hayahitaji kusubiri kama hili la Mnali, hasa ikizingatiwa kwamba wapo Watanzania lukuki wanaoweza kuongoza wilaya.

Viongozi wetu wanatakiwa wakati mwingine kuchukua maamuzi magumu na ya haraka kunapokuwa na jambo linalolalamikiwa na wananchi badala ya kulindana ama kusuasua.

La pili ambalo mimi nimejifunza ni kuungana na wale ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakishauri nyadhifa hizi za ukuu wa wilaya na mkoa, zisitolewe kisiasa hata kama viongozi hawa wanaitwa wawakilishi wa Rais.

Rais kwa kushirikiana na wasaidizi wake, hususan Waziri Mkuu hawezi kuwajua Watanzania wazuri waliotapakaa nchi nzima wenye sifa za kushika nyadhifa hizi na wakasaidia kusukuma maendeleo ya nchi mbele.

Mimi siungani sana na wale ambao wangependa nafasi za ukuu wa wilaya ama mkoa ziwe za kugombea kama ubunge, bali mimi ninaungana na wale wanaopendekeza zitangazwe, na wenye sifa waombe.

Huko nyuma, kwa mfano, chama cha mpira wa miguu nchini kiliendeshwa na katibu mkuu wa kuchaguliwa. Sasa hivi kinaendeshwa na mwajiriwa, aliyeomba na kuchaguliwa kutokana na sifa na uwezo wake ambapo akikiuka yale anayotakiwa kufanya anafukuzwa kazi.

Mimi ninaona kana kwamba mambo yanakwenda vizuri zaidi TFF kuliko zamani. Vivo hivyo, ingekuwa kwa wakuu wa wilaya na mikoa.

Nafasi ya mkuu wa wilaya ama mkoa ni nyeti. Zinataka watu wenye sifa ambao hawawezi kufanya mambo ya ajabu kama aliyofanya Mnali.